Mwanasoka George Weah aongoza katika uchaguzi Liberia

Mwanasoka maarufu George Weah anaonekana kuongoza katika uchaguzi mkuu nchini Liberia.

Mwanasoka George Weah aongoza katika uchaguzi Liberia

Mwanasoka maarufu George Weah anaonekana kuongoza katika uchaguzi mkuu nchini Liberia.

Kwa mujibu wa habari,ripoti zilizotolewa na siku ya Alhamisi zimeonyesha kuwa George Weah anaongoza katika uchaguzi uliofanyika siku ya Jumatatu.

Weah anaongoza katika majimbo 15 tofauti akifuatiwa na makamu wa rais kutoka chama tawala Joseph Boakai.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi amewataka watu watulie kwa sasa kwani matokeo kamili hayajatangazwa.

Mwenyekiti ametoa onyo pia kuhusu habari zinazorushwa mitandaoni kuhusu ushindi wa George Weah.

 Habari Zinazohusiana