Umoja wa Afrika wakemea matamshi ya Trump

Umoja wa Afrika wakemea matamshi ya kashfa yaliotolewa na rais wa Marekani kuhusu wahamiaji kuroka bara la Afrika ba Amerika-Kusini

Umoja wa Afrika wakemea matamshi ya Trump

 

Umoja wa Afrika wakemea vikali matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump kuhusu wahamiaji kutoka mataifa ya bara la Afrika na Amerika-Kusini ikiwemo Haiti na El Salvador.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Marekani, wakati wa mkutano kuhusu uhamiaji uliofanyika Alkhamis ikulu Washington, rais Trump  alitoa matamshi makali akisema kuwa mataifa ya bara la Afrika na Haiti ni mataifa machafu.

Msemaji wa Umoja wa Afrika Musa Faki amefahamisha kuwa Umoja wa Afrika unakemea vikali matamshi ya rais wa Marekani Donald Trump kuhusu mataifa ya bara la Afrika.Habari Zinazohusiana