Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Ujenzi wa bwawa Ethiopia

Ushirikiano baina ya Uturuki na Afrika

Nguvu ya nishati  nchini Ethiopia: Ujenzi wa bwawa Ethiopea

Imechambuliwa na Ibrahim Bachir Abdoulaye

Nishati ni kipengele muhimu cha uchumi wa nchi. Kwa sababu hii, ni muhimu kwa kila taifa kulinda usalama wa nishati. Nishati tena ni pendekezo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sekta na kwa maisha ya kila siku ya wanadamu. Wataalam wanatabiri kwamba mahitaji ya nishati kufikia 2040 yataongezeka kwa 60% katika nchi zinazoendelea. Wataalam pia wanasema kuwa 40% ya mahitaji hayo ya nishati ni kwa ajili ya usambazaji wa umeme.

Kwa maana hii, mojawapo ya sababu muhimu zaidi ya matatizo ya muda mrefu kama vile matatizo ya chakula nchini Afrika ,uzalishaji wa nishati ni tatizo mojawapo. Ingawa bara la Afrika lina uwezo mkubwa wa kuzalisha nishati, uwekezaji mkubwa wa kukidhi mahitaji hayo ya nishati hautoshi.

Kwa maana hii, mradi mkuu wa "Ujenzi wa bwawa", Ethiopia ambao ulianzishwa mwaka 2011, ni mfano wa kuigwa kwa nchi zote za Afrika. Kwa mradi huu, bwawa hilo litajumuishwa  katika orodha ya juu kabisa ya mabwawa duniani, Ethiopia itaendelea kuongoza katika uzalishaji mbadala wa nishati barani Afrika.Ujenzi wa bwawa hilo ambao ulianza kushughulikiwa mwaka 2013, upo Nile Blue, kilomita 40 kutoka mpaka wa Sudan. Upana wa bwawa ni mita 870 na urefu ni mita 175. Katika taarifa iliyotolewa na serikali ya Ethiopia mnamo Septemba mwaka jana, asilimia 60 ya utafiti kuhusu bwawa hilo umekamilishwa. Mradi huu umepangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu. Hata hivyo, itachukua miaka kati ya 5 na 7 ili kujaza bwawa. Kwa sababu bwawa linahitaji mita za ujazo bilioni 70 za maji ili kujaa. Megawati 6,450 za umeme zitazalishwa kutoka kwa mimea ya umeme  ili kuwekwa kwenye bwawa. Kwa rasilimali hii, Ethiopia itaweza kukidhi mahitaji ya nishati ya idadi ya watu ambayo inakaribia milioni 100 na kuongezeka siku kwa siku kufikia mwaka 2030.

Mradi huo wa Ethiopia unafikia gharama ya mradi wa Bwawa kuu, ambao ni karibu na dola bilioni 4.7, kwa mbinu zake yenyewe. Baada ya Benki ya Dunia na mashirika mengine ya kimataifa kukataa kuufadhili mradi huo, serikali ya Ethiopia iliweza kupunguza matumizi ya serikali na kubajeti mradi kwa kutumia rasilimali zake. Serikali ya Ethiopia imefanya uhamasishaji mkubwa wa kitaifa ili kufikia bajeti ya mradi huo. Wananchi wa Ethiopia pia walichangia  mradi huo.Ujenzi wa bwawa hilo ambao utakamilishwa kwa kıjitolea kwa watu wa Ethiopia, inatembelewa na maelfu ya wananchi wa Ethiopia kama ishara ya sifa ya taifa hilo.

Kwa kutambua mradi huu, ambao umekuwa katika ajenda ya serikali tangu miaka ya 1950, Ethiopia itaimarisha uongozi wake katika kanda.Vilevile, pamoja na mradi huu Ethiopia itakuwa kitovu cha nishati ya Afrika Mashariki.Baada ya mradi kukamilika; Sudan, Djibouti, Kenya, Sudan Kusini na Yemen zitakidhi gharama za mradi huo. Ethiopia inatarajia kupata milioni 2 kwa siku, milioni 730 kwa mwaka kupitia mradi huu, ambao ni muhimu sana kiuchumi. Mapato haya yatachangia kuziba pengö katika biashara nchini humo kwa gharama ya dola bilioni 9 za nchi.

Hata hivyo, kutokana na mradi huo kuwa Mto Nile, Ethiopia itakumbwa na matatizo fulani na nchi zinazofaidika na hilo. Kwa mfano, Ujenzi wa bwawa hilo Ethiopia, unaojulikana kama mradi wa Nahda huko Misri, umesababisha uhusiano wa Misri na Ethiopia kuwa mgumu. Misri, ikidai kwamba ina haki ya kihistoria kwenye Mto Nile, imekataa mradi huo kwa kudai kwamba bwawa likijengwa litapunguza maji ya mto Nile kwenda Misri. Ethiopia, hata hivyo, inasisitiza kuwa bwawa litatumika kwa ajili ya uzalishaji wa umeme tu na kwa hivyo mto hautathiri usambazaji wa maji. Wakati wa utawala wa Muhammad Mursi, wakati msingi wa Mradi huo ulipowekwa, Misri iliitahadharishia Ethiopia vita. Misri iliona mradi huo wa Ethiopia kama tishio la usalama wa kitaifa. Misri, chini ya utawala wa Uingereza mwaka 1929, ilisaini makubaliano na Ethiopia. Kwa mujibu wa makubaliano haya; Zaidi ya 60% ya haki ya kutumia mto wa Nile imepewa Misri.

 Pamoja na ujenzi wa mradi huu, Ethiopia inaonyesha kuwa inatumia haki yake ya msingi kulilinda taifa la baadaye.Misri nayo inasema kuwa ina haki juu ya mto huo kihistoria na kwamba suala hilo ni la kufa au kupona. Ethiopia, kwa upande mwingine, inasema kuwa haiwezi kuacha ujenzi wa bwawa wakati wowote.Kutokana na haya, Misri ilitaka kwenda kufanya mazungumzo na Ethiopia. Kwa hiyo, tarehe 15 Machi 2015, "Azimio la Kanuni" lilisainishwa kati ya Ethiopia, Misri na Sudan, Ethiopia ikaiondolea wasiwasi Misri. Hata hivyo, mnamo Novemba wa mwaka jana, Misri ilisisitiza kuwa ilihofia usalama wa taifa na hivyo kueleza wasiwasi wake kuhusu bwawa. Waziri wa Maji na Waziri wa Umeme wa Ethiopia Seleshi Bekele alijibu kuhusu wasiwasi huu wa Misri, na kutaja manufaa ya baadae ya mradi huo. Sudan imekuwa ikizidi kutatua mgogoro kati ya nchi hizo mbili hivi karibuni. Ethiopia, Sudan na Misri zilitoa uhakika ambao unahusu maendeleo yote kuhusiana na bwawa. Ethiopea imeihakikishai misri na Sudan kuwa itakuwa ikitoa taarifa kuhusu maendeleo yoyote ya bwawa hilo.Baada ya makubaliano yote Misri imeonekana kuwa itakuwa ikifaidika kwa asilimia 60 ujenzi wa bwawa hilo utakapokamilika.Ujenzi huo wa bwawa nchini Ethiopea ni mfano mzuri kwa nchi nyingine barani Afrika hasa katika sekta ya uwekezaji na uchumi.Baada ya ukamilika kwa ujenzi huo wa bwawa Ethiopea inatarajia uwekezaji wa hali ya juu barani Afrika.Habari Zinazohusiana