Kwa mara nyingine tena kipindupindu chaiandama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kipindupindu kimeendelea kuiandamana nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mara nyingine tena kipindupindu chaiandama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Kipindupindu kimeendelea kuiandamana nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa habari,kesi nyingi za mlipuko wa ugonjwa huo zimeonekana kwa kiasi kikubwa katika mji wa Mbujimayi.

Kulingana na ripoti zilizotolewa na gavana wa Kasai Alphonse Ngoyi Kasanji ni kwamba ni kesi 833 za kipindupindu zimeonekana ndani ya miezi minne iliyopita.

Zaidi ya watu mia moja wamepoteza maisha kutokana na janga hilo.

Kulingana na takwimu iliyotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) tarehe 14 Juni, kesi 11,699 za kipindupindu zimeonekana nchini tangu mwanzo wa mwaka.

Mji wa Mbujimayi wenye watu takriban milioni 2 ni sehemu inayoongoza kwa ugonjwa wa kipindupindu nchini DRC.

 Habari Zinazohusiana