Burundi, Rwanda na UNHCR  kukutana Geneva  kujadili kuhusu wakimbizi

Rwanda, Burundi na UNHCR kukutana mjini Geneva  katika mkutano kuhusu kurejeshwa kwa wakimbizi

Burundi.jpg

Mkutano kuhusu kurejeshwa kwa wakimbizi  kutoka Burundi waliokimbilia nchini Rwanda kufanyika mjini Geneva nchini Uswisi  mwanzoni mwa Oktoba.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Burundi na Rwanda, wawakilishi wao wanatarajiwa kukutana mjini Geneva kujadili kuhusu kurejeshwa kwa wakimbizi  kutoka Burundi waliokimbilia nchini Rwanda.

Taarifa kuhusu mkutano huo imetolewa  Alkhamis na wazibi wa mambo ya ndani wa Burundi Pascal Barandagiye.

Katika ziara yake nchini Burundi  Januari mwaka 2018, kamishna mkuu wa UNHCR Filippo Grandi anitoa ahadi kuwa ataandaa mkutano kuhusu wakimbizi  kutoka Burundi  walioko nchini Rwanda.

Burundi inaituhumu Rwanda kuwazuia wakimbizi  wanaotaka kurejea nchini Burundi kwa hiari ili izidi kujikusanyia  ruzuku ambazo zinatolewa na mashirika ya kutoa misaada kwa wakimbizi. Z

aidi ya wakimbizi 230 000 kutoka Burundi waliokuwa wamekimbilia nchini Tanzania wamekwisharejea nchini Burundi tangu Januari  mwaka 2016 ameendelea kufahamisha waziri wa mambo ya ndani wa Burundi.Habari Zinazohusiana