Rais Paul Kagame awatahadharisha wapinzani walioachwa huru nchini Rwanda

Rais wa Rwanda Paul Kagame awatahadharisha wapinzani walioachwa huru kwa msamaha wasijekurejea  gerezani

Rais Paul Kagame awatahadharisha wapinzani walioachwa huru nchini Rwanda

Rais Paul Kagame wa Rwanda amewatahadharisha wapinzani walioachwa huru kwa  msamaha wa rais nchini Rwanda.

Tahadhari hiyo imetolewa na rais Kagame kwa wapinzani wasije kurejea gerezani.

Rais  Kagame ameyasema hayo mbele ya wabunge wapya siku 3  baada  ya kuachwa huru kwa msamaha wafungwa  zaidi ya 2000 akiwemo  mpinzani Victoria Ingabire.

Mpinzani huyo alikamatwa mwaka 2010 na kuhukumiwa kifungo  mwaka 2013.

Rais Kagame amewataka wapinzani kuchukuwa tahadhari  na kusema kuwa wafungwa hao wameachwa huru kwa kuwa nao ni raia ambao wanaweza kuwa na mchango wa kujenga taifa na sio kwa shinikizo la aina yeyote ile.Habari Zinazohusiana