Kuhusu TRT

TRT – Muhtasari

 

Idhaa ya redio na Televisheni ya Kituruki (Turkish Radio & Television Broadcasting Corporation)

 

Idhaa ya Matangazo ya kwanza na ya kipekee Uturuki ya TRT , ilianzishwa tarehe 1 Mei mwaka 1964. Kituo cha redio kilichoanza kurusha matangazo yake tarehe 5 Mei mwaka 1927, kimekuwa chini ya TRT. Kwa kutufikisha sehemu tofauti kote duniani, kituo hiki kilijiunga na vyengine mwishoni mwa miaka ya 1960. Ilikutana na Televisheni ya Uturuki kwa mara ya kwanza tarehe 31 Januari mwaka 1968 kupitia TRT. Pamoja na uzoefu wake wa miaka 81 kwa redio na miaka 40 kwa televisheni, TRT ni kumbukumbu muhimu katika historia ya Jamhuri ya Uturuki. Kwa tajriba na uwajibikaji wake, imekuwa nguzo ya kutegemewa na alama ya umoja wetu.

 

Katika kipindi cha matatizo na changamoto nyingi, utangazaji ulianza kwenye kituo kidogo cha Mithatpaşa katika mazingira duni. Hata hivyo, kwa juhudi za wafanyakazi ili kukwepa vikwazo waifanikiwa kupata mafanikio ndani ya muda mfupi hatimaye TRT ikapata sehemu ya kudumu na kuwa kituo ambacho taifa la Uturuki linajivunia. Katika kipindi cha sasa, ambapo TRT imekuwa ni kituo cha mafunzo ya utangazaji na sehemu inayotegemewa kwa matangazo Uturuki, imeelimisha na kuzalisha watayarishaji wengi wa vipindi vya televisheni waliofanikiwa. Kwa hiyo imechangia kuwepo kwa vipindi vya kuvtia na kufurahisha.

TRT haikubaki kuwa ‘Shirika la Utangazaji ‘ la redio na televisheni pekee, bali kilikuwa ni kituo cha mafunzo. TRT ilikuwa muhimu kwa mipango yake ya kuelimisha na kutoa vipindi vya vinavyofunza katika matangzo yake ya habari.

 

Kwa uwezo wake wa kuimudu bendera yake, TRT imeweza kuwa kituo sahihi cha habari za kuaminika na vipindi bora kwa kuzingatia kanuni za utangazaji kwa umma hadi kufikia kutambulika kama moja wapo ya vituo bora duniani.

Tunaweza kuelezea chanzo cha mafanikio haya kama ifutavyo;

 

Uwajibikaji na Uaminifu katika Utangazaji

 

TRT imefnikiwa kuwa na ofisi nyingi muhimu kutoka Marekani hadi Ulaya, Asia hadi Mashariki ya Kati na Caucasia, ambavyo vina umuhimu mkubwa kwa Uturuki na Dunia nzima kupitia mahojiano ya MAREKANI – Washington, UBELGIJI – Brussels, MISRI– Cairo, UJERUMANI – Berlin, TRNC – Nicosia, AZERBAIJAN – Baku, TURKMENISTAN – Ashgabat, UZBEKISTAN – Tashkent.

 

Waandishi wa habari wenye uzoefu, wanaofanya kazi katika kitengo maalum waliopo kwenye ofisi za Istanbul, Izmir, Antalya, Çukurova, Diyarbakır, Erzurum and Trabzon ikiwemo ofisi ya makao makuu ya Ankara, mahojiano na wanahabari wa ndani, na mitandao ya habari iliyopo kila kona ya Uturuki.

Alama ya ‘’Uaminifu’’ kwa watazamaji na wasikilizaji wake na lengo la habari za kuaminika.

 

Matangazo kwa kila umri na utamaduni

 

Elimu na Utamaduni, muziki na burudani, vipindi vya watoto na michezo , mijadala, makala, michezo ya kuigiza, matangazo ya filamu za hali ya juu na zilizo bora. Kuwafikia watazamaji mbali mbali wenye elimu tofauti, umri tofauti na ngazi tofauti katika jamii na kiuchumi. Matangazo yaliyofikia kiwango cha kimataifa na kuungwa mkono katika uongozi wake.

Kuweza kutazamwa kila pembe ya dunia kupitia runinga zake 7 : 4 za kiatifa, 2 za kimataifa na 1 ya mikoani.

Runinga hizi ni ;

 

 

TRT 1: Idhaa ya Familia, masaa 168

 

TRT 2: Taarifa za habari, maelezo, utamaduni na sanaa, masaa 168

 

TRT 3: Idhaa ya vijana na watoto, masaa 54

 

TRT GAP: Matangazo ya mikoa ya Mashariki na Mashariki ya Kusini, masaa 69

 

 TRT 4: Elimu na Muziki, masaa 139

 

TRT INT: Matangazo ya ulimwengu, masaa 168

 

TRT TURK:Matangazo ya Asia ya kati na Caucasia, masaa 119

 

Uwezo mkubwa wa kuunganisha Ulaya na Asia kwa njia ya satelaiti za kimataifa na vituo viwili ardhini. Kuwa na upeo mkubwa wa kuwasilisha maendeleo ya nchi na masuala ya dunia kwa taarifa za undani na ufafanuzi zaidi kote katika nyanja za kitaifa na kimataifa.

Kupitia runinga ya TRT-TURK, imefanikiwa kuunga jamii kwa matangazo ya Caucasus na Mashiri ya Kati, na kutambulisha Uturuki na Waturuki na kuwezesha lugha inayounga mataifa ya jamii za Jamhuri ya Uturuki, ni kuimarisha ushirikiano katika kuendeleza utamaduni na masuala ya kibiashara.

Kuchangia katika kuimarisha uhusiano wa utamaduni baina ya waturuki wanaoishi katika nchi za kigeni kupitia matangazo ya TRT-INT yanayorushwa hasa kwa waturuki wanaoishi Ulaya na kuwafikia kila pembe ya dunia.

Kwa kuimarisha , TRT-INT, kiwango chake kimeongezeka na kuzidisha upinzani dhidi ya vituo vyeninge vya habari katika nyanja za kimataifa.

Televisheni za TRT zinazotengenezwa kwa sasa.

 

Kutoa huduma kwa wananchi wanaozungumza lugha tofauti na maeneo yaliyokuwa na ushirika katika lugha hizi. Jitihada za kuanzisha runginga mpya zinazotangaza kwa lahaja za Kirmançi na Zaza. Lengo la matangazo kwa lugha za Kiajemi na Kiarabu ili kumarisha uhusiano kati ya watu wanaozungumza lugha hizi.

Juhudi za kuanzisha ‘’Runinga ya Watoto’’ na uwezo wa kuwafikia watoto Uturuki na kote duniani.

 

Miaka 80 ya uzoefu katika redio

 

Redio za TRT zimekuwa chaguo la watu Uturuki kwa vituo vyake 4 kitaifa, 5 mikoani na redio ya utalii (Tourism Radio). Wafanyakazi wenyeuzoefu, vikundi vya kwaya katika kila tawi la mziki, wasanii wenye vipaji, vilabu vya watoto na vijana, kumbukumbu zilizobobea, matangazo yanayosaidiwa kwa mitambo ya tarakilshi, vituo vyenye vifaa vya teknolojia ya sasa, ustadi wa hali ya juu na mipango kabambe kwa ajili ya matangazo katika hali ya kisasa.

 

Idhaa za redio

 

Radio 1: Idhaa ya elimu, utamaduni na taarifa za habari. Imekuwa ni muhimu kwa wasikilizaji wake kwa miaka 8 ya huduma ya vipindi vinavyohusiana na masuala ya kimaisha pamoja na taarifa za habari kila saa.

Radio 2 (TRT FM): Idhaa ya miziki maarufu iliyokuwa na nyimbo za asili za kituruki bora, nyimbo za kitamaduni na miziki ya kizazi kipya.

Radio 3: Miziki ya jadi, jaz na opera.

Radio 4: Miziki ya asili ya Kituruki na miziki ya jadi.

Idhaa hizi zote nne za redio zipo hewani masaa 24 kote Uturuki na duniani kupitia mitandao.

Redio tano za matangazo ya mikoani

Trabzon Radio, Erzurum Radio, GAP-Diyarbakır Radio, Antalya Radio na Çukurova Radio... Tourism Radio pia ina umuhimu sana kwa hudumia watalii wakituruki na watalii wa nchi zengine walioko Uturuki.

 

Matangazo ya redio kwa lugha 29 ulimwenguni

 

Sauti ya Uturuki inaimarisha mawasiliano baina ya waturuki wanaoishi nchi za kigeni na wale waliomo nchini kwa kurusha matangazo kwa lugha 29 ikiwemo kituruki,  hivyo basi, kueneza taarifa katika maeneo yote ya Uturuki na duniani.

 

Kuenea kwa Mawasiliano Duniani kupitia Matangazo

 

‘’Uaminifu na mtazamo wa siku zijazo’’ katika taasisi za utangazaji unaoenea kwa kasi kutokana na ubunifu wa huduma za vyombo vya habari zinazosababishwa na uzoefu, uwezo na maarifa yanayotakana na yale ya zamani.

Mkusanyiko huu umechangia pakubwa na kuvutia mafanikio yanayozidi kuendelea katika miundombinu  ya kiufundi. Tunarusha matangazo ya ndani na nje ya mipaka ya nchi kupitia njia ya visambazi vyenye nguvu za Mega Watts 61 kwa televisheni na Mega Watts 22 kwa redio amabazo ni bora zaidi ya nguvu zinazotumika katika vituo vyote vya kibinafsi Uturuki.

Hivi ndivyo vituo vyetu vya satelaiti vinavyorusha matangazo ya redio na televisheni kupitia  satelaiti ya TURKSAT 2A na TURKSAT 1C (3A).

Mbali na hayo, TRT ni taasisi iliyokuwa na vituo 42 vya utayarishaji na utangazaji na moja ya vituo hivyo kinapatikana ndani ya ofisi ya Berlin.

Vyombo  9 vinayorusha matangazo hewani katika vipindi vya televisheni

Satelaiti ndogo ya mifumo ya viunganishi na vielekezi vya televisheni

Satelaiti ndogo zisizokuwa na mifumo ya viunganishi zilizoko Turkmenistan and Diyarbakır,

Vyombo vinavyohusika na satelaiti ya redio ya mahojiano.

Vituo 55 vya utayarishaji na utangazaji wa vipindi vya redio.

Vyombo 9 vyenye mifumo ya viunganishi vilivyoungwa na satelaiti ya redio na televisheni.

Magari 5 ya kurusha matangazo na mahojiano hewani.

Na magari 6 ya jenereta za kubebwa.

Vipindi vya majaribio hurushwa hewani masaa 24 mfululizo Ankara, Istanbul na Izmir.

 

 

TRT katika Mtandao

 

Inalenga kuhudumia na kukidhi matarajio ya watazamaji wake katika mfumo wa dijitali, na kutoa fursa za kiteknolojia kwa umma. Imeweza kuleta miradi mengi muhimu katika jamii kwa kipindi cha muda mfupi.  Tovuti rasmi ya http://www.trt.net.triliweza kuvumbuliwa tarehe 1 Mei mwaka 1999. Vipindi vya redio na televisheni vinapatikana katika mtandao kwa watazamaji na wasikilizaji wanaweza kufikia huduma ya TRT.  Isitoshe, tovuti inasaidia kwa utafiti wa taarifa muhimu kutoka Uturuki na duniani ili kupata taarifa za maendeleo ya kiuchumi na zinazohusiana na sekta za biashara, kutoka nyanja zote za michezo, utabiri wa hali ya hewa  na vipindi vya matangazo vya redio na televisheni.

Matangazo ya TRT mtandaoni yamepiga hatua kubwa na kuanza juhudi za kutayarisha tovuti kwa lugha tofauti. Taarifa za kigeni zitatolewa kwa lugha 11 kwa kuanzia na baadaye kuna mikakati ya kurusha matangazo  kwa lugha zote kupitia Sauti ya Uturuki.

 

TRT Archive, (kumbukumbu ya TRT) , ni kumbuku ya Visual-Oral ya Uturuki

 

Kuna uhifadhi wa kumbukumbu uliochangia katika kuimarisha historia ya Jamhuri ya Uturuki.

TRT pia inasifa ya kudumisha matumizi ya teknolojia ya kisasa duniani.

Kumbukumbu na taarifa hizo za kihistoria huhamishwa na kuwekwa katika vyombo vya habari vilivyo na mfumo wa kidijitali kupitia uchambuzi na ufundi wa hali ya juu.

 

Soko la TRT

 

Soko la TRT linatoa huduma ya vipindi na muziki kupitia njia ya kutizama, kusikia na kuchapisha.

 

Makala ya redio na televisheni ya TRT

 

Makala ya redio na televisheni ya TRT, ambayo husambazwa kila mwezi tangu Novemba mwaka 1997, yameleta maendeleo ya kisasa katika taasisi na mwelekeo mzuri katika utayarishaji mkuu wa vipindi vya redio na televisheni kwa undani. Makala yanayochapisha maudhui ya kuvutia katika mawasiliano, utamaduni na sanaa, pamoja na michezo.

 

TRT,  Tegemeo la Mashirika Makuu

 

TRT imekuwa kituo cha kudumu katika kuhudumia mashirika ya kimataifa na kuchangia amani duniani. Kwa mfano Sherehe ya Kimataifa ya Watoto ya tarehe 23 Aprili, ambapo watoto kutoka sehemu tofauti, lugha tofauti na dini mbali mbali hujumuika pamoja Uturuki kwa muda wa siku kumi.

 

TRT pia imekuwa na mchango mkubwa katika maandalizi makubwa kama vile mashindano ya kuimba ya  Eurovision Song Contest,  mashindano ya dunia ya World Cup Championship, mashindano ya michezo ya Olimpiki na mashindano ya michezo ya vyuo vikuu duniani.

Kwa kifupi, Uturuki imefungua njia kwa wote duniani na vile vile kote duniani wamefunguliwa njia ya Uturuki. Yote haya ni kwa sababu ya herufi tatu za TRT.

 

Wanachama

 

EBU– European Broadcasting Union
ABU – Asia-Pacific Broadcasting Union
HFCC/ASBU – International High Frequency Broadcasters Coordination Group
ABU-HFC – ABU High Frequency Broadcasters Coordination Group IMC – International Music Council
EIM – European Institute of Media UNESCO Turkish National Committee Turkish National Council of Press
CMCA – Centré Méditerranéen de la Communication Audioviseulle
 

Kwa maelezo zaidi: (http://trt.net.tr/Kurumsal/Tarihce.aspx)