TRT TV

Kwa kutoa huduma yake duniani ya taarifa sahihi kwa kupitia vyombo vyake vya habari vilivyojaa runinga za kitaifa na kimataifa, TRT inatoa matangazo ya vipindi vinavyohusiana na elimu, utamaduni, makala maalum, michezo ya kuigiza, michezo, muziki na burudani kwa watazamaji wa umri wote wanaofikia idadi ya asilimia 99.9% ya Anatolia nzima na zaidi.
TRT inafanya matangazo kwa lengo la kutoa taarifa sahihi, za kueleweka, na habari za uhakika kwa watazamaji wake wote katika jamii pasi na kujali umri wao, taaluma, kiwango cha elimu wala utamaduni wao na inachangia pakubwa maendeleo ya elimu na utamaduni kwa kuelimisha na burudisha na kuhifadhi mil ana desturi za taifa.

Ni runinga ya familia. Runinga inayotazamwa zaidi nchini Uturuki ya TRT-1, inaonyeshwa kwa mfumo wa kifamilia na kuhudumia watazamaji wote nchi nzima kwa vipindi vya elimu, utamaduni, michezo ya kuigiza, muziki, burudani, michezo na taarifa za habari. Kwa kuteka asilimia 99.9% ya Uturuki, TRT-1 inapatikana Uturuki nzima nzima na kote duniani kupitia mtandao. Mhudumu wako wa miaka 43.

TRT-NEWS ni runinga inayowaletea watazamaji matukio mbali mbali yanyojiri, ufafanuzi wa michezo, vipindi vya utamaduni na sanaa kwa ukamilifu. Tumia haki yako kupata taarifa sahihi za habari. Runinga ya taarifa za habari ya TRT-NEWS ipo kila sehemu.

Runinga inayotumiwa na TRT-GAP na TGNA TV. Mashindano ya michezo ya Uturuki na dunia pamoja na vipindi vya michezo mbali mbali vinaweza kutazamwa moja kwa moja katika runinga hii.

Kwa kutekeleza mahitaji na matakwa ya watu wanaoishi Mashariki na Mashariki ya kusini mwa Anatolia, TRT-GAP inalenga kuimarisha maendeleo ya kiuchumi na viwango vya elimu kwa kuonyesha vipindi vya muziki, elimu, utamaduni, burudani, michezo na makala maalum. TRT-GAP ni sauti kuu ya watu wa mikoani.

Runinga inayotumiwa na TRT ya Watoto na TRT ya Shule.

Baada ya kuzinduliwa rasmi mwezi Oktoba mwaka 2010, TRT-ANATOLIA inachukua sehemu kubwa katika kumbukumbu ya TRT na matayarisho mengine yanayotokana na ushirikiano wa runinga za TRT. Wakati huo huo, vipindi vya runinga za mitaani na mikoani vinavyohusiana na maadili, mila na utamaduni, vinawakilishwa kwa kupitia runinga hii.

Kwa runinga yake ya kimataifa kwa lugha ya kikurdi, TRT-6 imechangia pakubwa uhusiano wa Uturuki wa kimataifa na hasa zaidi wa mikoani. Runinga ya familia ya Kikurdi ya TRT-6, inayolenga kuimarisha amani na uadilifu nchini kwa matangazo yake yanayozingatia kanuni za kisasa kwa watazamaji wa kila umri, ilianza shughuli zake za kazi mwezi Januari mwaka 2009.

Runinga inayokidhi mahitaji ya watoto wa Uturuki kupitia kuonyeshwa kwa filamu za uhuishaji,muziki, taarifa na michezo kwa lengo la kuimarisha malezi bora ya kimwili, kiakili na kimaadili kwa vizazi. TRT ya Watoto (TRT Children) ambayo ni mwongozo katika kuwakuza watoto na kuwajibika kwa malezi bora pamoja na kuelewesha utangazaji wa kisasa, imekuwa ni jicho pevu ulimwenguni la kanuni za ufundishaji zinazokubaliwa. Runinga hii inayotumia lugha ya kituruki sahihi na ya kiwango cha watoto, imechangia kuleta ufahamu wa kitaifa kwao kwa kupitia vipindi vyake vya kuburudisha na kuelimisha.
http://www.trtcocuk.com/

Runinga ya TRT inayorusha matangazo kwa lugha ya Kituruki sehemu nyingi nchini na duniani kwa madhumuni ya kutambulisha Uturuki pamoja na Waturuki kwa kupitia taarifa za habari na vipindi vya utamaduni na sanaa. Vile vile inaimarisha uhusiano baina ya waturuki wanaoishi katika nchi za kigeni na nchi yao. TRT-TÜRK ni runinga madhubuti kwa uhusiano kati ya raia wa Uturuki wanaoishi nje na Uturuki, ni kipenzi chao katika dhiki na faraja, na huwafikia popote walipo duniani.

Baada ya kuzinduliwa mwezi Machi mwaka 2009, runinga hii inahudumia sehemu kubwa ya kijogrfia kutoka Mashariki ya mbali mpaka Balkans kuanzia Uzbekistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Turkmenistan, Azerbaican, Bosnia –Herzegovina, Albaniana Uturuki katika lugha ya kipekee inayofahamika kwa lengo la kuimarisha jamii moja na maelewano baina ya Uturuki na nchi zinazozungumza lugha ya Kituruki. AVAZ ambayo ina maana ya SAUTI katika lahaja nyingi za Kituruki, inawakilisha eneo lenye watu milioni 250 kutoka Mashariki ya Kati mpaka Caucasus katika nchi 27 na jamhuri za mataifa 13 kama sauti moja ya jamhuri za mataifa yanayozungumza Kituruki.

Runinga ya makala maalum inayohabarisha dunia na Uturuki kwa kuonyesha makala tofauti ikiwemo ya kijamii, viumbe asili, mazingira, sayansi na teknolojia kutumia lugha ya Kiingereza, Kijerumani, Kifaransa, Kirusi na Kituruki. Inaunganisha mambo ya kale na yala yaliyokuwa usoni na kufuatilia maendeleo ya mazingira. Runinga hii ilizinduliwa tarehe 17 Oktoba mwaka 2009.

Runinga hii hukutanisha dunia na muziki wa Kituruki kupitia makala ya mashindano, maonyesho ya michezo, makala maalum ya muziki, maonyesho ya muziki na miziki iliyokuwa kwenye chati ya 10 bora. Baada ya kuzinduliwa mwezi Novemba mwaka 2009, runinga ya TRT-TÜRK huonyesha miziki ya asili na kitamaduni ya Kituruki pamoja na miziki ya kisasa.

Runinga hii inalenga kuimarisha uhhusiano wa Uturuki wa jamii ya kimataifa hasa kwa nchi jirani. Inatangaza kwa lugha moja inayowajumuisha Uuruki na mataifa ya Uarabuni na kuifikia jamii nzima pasi na kujali umri wala jinsia, kwa matangazo yanayohusiana na vijana, wanawake, afya, uchumi, michezo, muziki, habari, utamaduni, sanaa, vipindi vya burudani pamoja na michezo ya kuigiza na mambo ya kisasa. Nchi 22 za Kiarabu zinazojumlisha idadi ya watu milioni 350, ndio walengwa wa runinga hii inayojizatiti kuimarisha uhusiano baina ya Mataifa ya Waarabu na Uturuki.

Runinga hii inatoa huduma ya matangazo ya vipindi vya michezo, makala maalum na filamu kutokana na ubora wake katika utangazaji wa hali ya juu kwa mfumo wa HD. Baada ya kuzinduliwa mwezi Juni mwaka 2010, TRT HD iliyotangaza Kombe la Dunia la mwaka 2010, pia itarusha matangazo ya michezo ya olimpiki ya misimu yote.


Runinga hii iliyoanza kufanya kazi mwezi Agosti mwaka 2010, imebeba sifa kwa matangazo yake muhimu katika njanja mbali mbali za michezo na mashindano ya kitaifa na kimataifa yanayoendelea au yaliyorekodiwa.