Miaka 15 jela kuvaa jezi ya Barcelona iliyofadhiliwa na Qatar

Miaka 15 jela kuvaa jezi ya Barcelona iliyofadhiliwa na Qatar katika nchi za Milki ya Kiarabu

Miaka 15 jela kuvaa jezi ya Barcelona iliyofadhiliwa na Qatar

Mamlaka za Milki za kiarabu zatangaza kuwa raia watakaovaa jezi za Barcelona zilizobeba jina na Qatar wataweza kuhukumiwa miaka 15 jela .

Mashabiki wa soka kutoka Milki za Kiarabu watajiingiza matatani wakivalia t- sheti za klabu ya Barcelona zilizo na lebo ya Qatar Airways .

Aidha mamlaka hiyo ilifaamisha pia watakapatikana na hatia hiyo watakatwa faini ya takriban dola elfu 135 au jela miaka 15.

Mnamo mwaka 2011 idara ya uwekezaji ya michezo ya Qatar ilifanya mkataba na klabu bingwa ya kimataifa ya Barcelona na kutengeneza jezi za timu hiyo iliyobeba jina la Qatar Airways .

Klabu hiyo ya Uhispania ni maarufu na inapendwa sana katika mataifa ya Ghuba ya kiarabu na uamuzi huo ulizua hasira baina ya mashabiki walioelezea hisia zao kupitia mitandaoni.

 Habari Zinazohusiana