May azungumzia shambulizi la Finsbury

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa hotuba kufuatia shambulizi la Finsbury.

May azungumzia shambulizi la Finsbury

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametoa hotuba kufuatia shambulizi la Finsbury.

Bi May amesema kuwa kwa mara nyingine Uingereza imekumbwa na shambulizi dhidi ya waislamu.

Bi May ameyasema hayo wakati alipoutembelea msikiti karibu na eneo la tukio.

Katika hotuba hiyo Bi May amesema kuwa magaidi wana nia ya kuisambaratisha nchi kwa mashambulizi ya hapa na pale lakini Uingereza itahakikisha inadhibiti matendo hayo.

Shambulizi hilo lilitokea muda mchache baad ya waumini wa dini ya kiislamu kufungua swaum zao.

Mwenyekiti wa mji huo pia ameongezea kwa kusema kuwa shambulizi hilo halikuwa la haki kwani limeathiri watu wasio na hatia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

 Habari Zinazohusiana