Kura ya maoni katika jimbo linalotaka kujştenga na serikali ya Baghdad

Kura ya maoni katika jimbo linalotaka kujştenga na serikali ya Baghdad

Kura ya maoni katika jimbo linalotaka kujştenga na serikali ya Baghdad

Rais wa jimbo la kikurdi la Irak, Mesut Barzani, alitangaza rasmi kuwa jimbo hilo litapiga kura ya maoni ya kujitenga kutoka Irak, na kuwa nchi huru, tarehe Septemba 25, 2017.

Baadae, bunge la mkoa wa  Kirkuk lilitangaza kuwa mkoa huyo utajiunga na kura hiyo ya maoni.  

Hata hivyo, jimbo hilo la Kikurdi halikuonesha nia yake ya kushirikiana na umoja wa mataifa . Licha ya Chama cha rais wa jimbo hilo, bwana Barzani, vyama vingine bado havijatoa taarifa rasmi kuwa watajiunga na kura hiyo ya maoni au laa.

Jamii ya warabu na waturkmen, wanaoishi jimbo hilo, bado hawajaonesha msimamo wao kuhusu kura ya maoni ya kujitenga. Jamii hizo mbili hazina makundi ya wapiganaji ili waweze kutetea na wenyewe haki zao, ila kinachidhihirika,mustakabali wa jimbo hilo ni kitandawili, maana , jamii hizo mbili zitakapoamua kupigania haki zao, mgogoro mwingine utazuka katika jimbo hilo.

Nadhani kura hiyi ya maoni; ikiwa hakuna kikwazo dhidi yake na ikapigwa; matokeo yake ni kusababisha vita vikubwa katika eneo hilo . Umuagaji damu sawa na ule uliotokea baada ya mkataba wa Berlin mwaka 1938, unaweza ukaibuka tena katika kanda hiyi ya mashariki ya kati.

Kura ya maoni itakaopigwa katika jimbo la wakurdi wa Irak, italeta mgawanyiko na mgogoro mkubwa katika kanda kwa ujumla. Kwanza kabisa, ni lazima niseme hili; sio halali kwa jamii ya wakurdi nchini Irak kujitenga, sababu leo jimbo lenyewe hilo, lina rais wake anaetoka jamii ya wakurdi. Na jimbo hilo la wakurdi wa Irak, lina uhuru na mamlaka vyake.

Serekali ya Irak haishinikizi wala kubugudhi jimbo la wakurdi wa Irak. Kwa hiyo hakuna haja wala uhalali wowote wa wakurdi wa Irak kujitenga. Ikiwa madai ya kujitenga yatachukuliwa  kuwa halali kwa njia hii, itashawishi maeneo  mengine kujitenga.

Hali ya kuwa, sheria ya kimataifa inahimiza umoja na kuungana kwa nchi. Sheria hii ni dhamana ya amani na utulivu wa  kimataifa. Kujitetea ni haki , endapo umoja , na haki za wananchi viko hatarini. Mchakato mzima wa kura ya maoni una matatizo makubwa hasa wa kisheria.

Aidha, hata miongoni mwa Wakurdi wa jimbola Irak, wengi wao wanapinga kupigwa kwa kura hiyo ya maoni.

Uamuzi uliofanywa na bunge la mkoa wa Kirkuk, pia ni kinyume na sheria na hauna umuhimu wowote. Uamuzi huu ni, kwanza kabisa, kinyume na sheria ya sasa ya Irak, hasa katiba. Hakuna wajumbe wa Turkmen, na jamii za Kiarabu walioshiriki kikao hicho. Wanachama 24 kati ya 26 ya wakikurdi , 21 kati yao ndiyo waliopiga kura ya ‘ndiyo’. Uamuzi wa bunge la mkoa wa Kirkuk ulichukuliwa na wakurdi tu, na uamuzi huo hauendi sambamba na katiba ya sasa ya Irak.

Eneo  ambalo Barzani na washirika wake sasa wanadhibiti, na kutangaza uhuru ni eneo halisi  la waTurkmens toka enzi za kale. Kudhibitiwa leo na Barzani kwa eneo hilo, haibadili ukweli wa mambo. Wengi wa wakazi wanaoishi vitongoji karibu na mipaka ya kanda hiyo ni waturkmen.

Ikiwa uamuzi wa kura ya maoni ya kujitenga itapitishwa, basi haki ya kujitegemea kwa Waturkmen na makabila mengine, ikiwemo na makundi ya madini tofauti , itakuwa ni mwanzo wa kupotea kwa makabila hao. Ikiwa uamuzi huu utakubalika, maombi yote ya makundi mengine kujitenga, yatakuwa halali kulingana na sharia ya mwaka wa 1990 .

Ikiwa wakurdi wana haki ya kujitenga na Irak, basi makundi yote ya kikabila na ya kidini wanaoishi Irak yana haki ya kufanya hivyo.

Ikiwa kura ya maoni itapigwa katika hali hiyi, na uamuzi wa kujitenga ukaidhinishwa , Waturkmen wa Irak  wanaweza kutia kwenye ajenda yao, uandalizi wa kura ya maoni ya kujitenga na wao kutoka  Irak. Aidha, siku zijazo,  Jamhuri ya Uturuki pia inaweza kujikuta kwenye ajenda ya kusaini makubaliano ya ushirikiano dhidi ya majimbo ambayo yanatishia umoja wa Uturuki.Habari Zinazohusiana