Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Rais Recep Tayyıp Erdoğan na majukumu ya Umoja wa Mataifa

Uturuki na mtazamo wa Mashariki ya Kati

Tunapochunguza Mkataba wa Umoja wa Mataifa (UN); Tunaona kwamba haki ya msingi ya taasisi ya Umoja wa Mataifa ni kuzuia vita, kudumisha  amani, kupiga vita matatizo yoyote ya kisiasa, kisaikolojia, kijamii, kiuchumi na kiutamaduni ambayo yanahatarisha usalama wa kimataifa.

Malengo haya ya msingi, na kanuni, zilijitokeza kwa lengo la kuzuia kuibuka kwa migogoro mipya,  baada ya vita viwili vya dunia. Umoja wa Mataifa umeundwa na taasisi sita.

Ambazo ni : Mkutano Mkuu, Baraza la Usalama, Baraza la Uchumi na Jamii, Halmashauri ya Usimamizi, Mahakama ya Kimataifa ya Haki za binadamu,  na katibu mkuu.

Katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, wanachama wote wa Umoja wa Mataifa hukutana huko New York, kila Septemba, kujadili masuala na mizozo ya kimataifa.

Pia washirika hupeana hoja, na maoni juu ya marekebisho ya Umoja wa Mataifa, ili kuboresha zaidi mienendo yake ya sasa, na siasa za kimataifa.

Mkutano huu wa kila mwaka, pia unaruhusu viongozi kufanya mikutano yao mbalimbali wakati wa vikao vya mikutano rasmi.

Mazungumzo mengi yasiyo ya rasmi kati ya nchi, na mazungumzo ya viongozi wa nchi wanachama wenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani,  huchangia sana na hubadilisha mwenendo wa sera na maoni duniani.

Leo, Umoja wa Mataifa una wafanyakazi takriban 40,000 kwenye taasisi  mbalimbali ulimwenguni kote. Bajeti ya kila mwaka ni dola bilioni 40.

Umoja wa Mataifa, jeshi lake lina askari wapatao elfu 100 , pia huendesha harakati kadhaa za kuhifadhi amani katika maeneo tofauti yenye migogoro .

Licha ya kutokuwepo jukumu la kulinda amani kwenye  mkataba wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Mataifa ulijishughulisha na kazi ya kulinda amani kuanzia  miaka ya 1950. Idadi ya shughuli hizo, imeongezeka kwa kasi zaidi katika kipindi hiki cha miaka ishirini na mitano iliyopita, ikilinganishwa na zama za vita baridi, kutokana na mvutano unaoongezeka miongoni mwa madola yenye nguvu zaidi duniani, na migogoro ya kivita inaokumba nchi tele duniani.

Hata kama palijitokeza mgawanyiko, na mvutano wa sera na mawazo kuhusu kuundwa kwa Shirikia la Umoja wa Mataifa, , limekuwa na jukumu muhimu sana katika ushirikiano wa kimataifa, na kuwezesha utendajikazi wa ushirikiano huyo.

Mashirika ya kimataifa yamekuwa watendaji muhimu katika nyanja mbali mbali za uendeshaji  wa nchi. Umoja wa Mataifa umeweza kuimarisha ushirikiano wa kimataifa .

Kwa upande mwingine, baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa mwaka wa 1945, siasa za kimataifa ziliundwa ili kutengeneza na kulinda sheria na taasisi za kimataifa kwa miongo kadhaa baada ya  vita vya pili vya dunia. Kwa sababu hii, Umoja wa Mataifa haujawahi kuwa taasisi ambayo inaweza kukomesha migogoro.

Kazi kuu ya Umoja wa Mataifa, ni kuleta ufumbuzi wa mizozo na migogoro ya kimataifa kwa urahisi na gharama nafuu. Pia kuna hatua ambazo zinahitajika kuchukuliwa, ili kuhakikisha hili. Wajumbe watano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanapaswa kuacha kutumia Umoja wa Mataifa kama chombo cha kulinda maslahi yao na kuendelea kudumisha ushawishi wao duniani. Vinginevyo, kazi za Umoja wa Mataifa, na michango kwa ajali ya kulinda amani na usalama wa kimataifa zitabaki ni ndoto.

Pamoja na mapungufu yake yote, na kutofaulu, Umoja wa Mataifa unaonekana kuwa chombo cha kimataifa chenye uhalali mkubwa, katika uwanja wa kimataifa. Ili uhalali huu, wa Umoja wa Mataifa udumu, nchi tano zenye neno la mwisho, au veto, lazima zihishimishe na zizingatie masharti na mkataba wa Umoja wa Mataifa bila kuangalia maslahi yao.

Pamoja na mageuzi ya kufanyika katika kipindi kijacho, mashirika ya Umoja wa Mataifa yanahitaji kufanyiwa mageuzi, ambayo yanaendena na hali halisi ya nchi ambazo sio za kimaghribi.

Umoja wa Mataifa lazima utafakari mienendo mipya,  inayojitokeza katika ulimwengu wa leo.

Ujerumani, India, Japani, Brazili, Uturuki na nchi nyingine zinaweza kujiunga na Baraza la Usalama kwa kipindi cha miaka miwili tu kwa mzunguko, wakisubiri kuchaguliwa na Mkutano Mkuu tena.

Hata hivyo, wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ni nchi zenye kiwango sawa, na nchi hizi bado wana haki ya kura ya veto, kama vile Uingereza na Ufaransa. Hali hiyi ni wazi kuwa siyo ya haki.

Ufumbuzi wa haraka wa udhalimu dhidi ya nchi kama vile Ujerumani, India, Japan, Brazili, Uturuki inapaswa pia kufumbuliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kama Rais wa Uturuki , Recep Tayyip Erdogan, anavyosema kila akiipata fursa: "Dunia ni kubwa kuliko nchi tano."Habari Zinazohusiana