Uturuki na mtazamo wa mashariki ya kati

Uturuki na mtazamo wa mashariki ya kati

Uturuki na mtazamo wa mashariki ya kati

 

Ushirikiano juu ya suala la kuhakikisha udhibiti wa migogoro katika mkutano wa Astana, ambao ulifanyika  Septemba 15, unaendelea kuimarika. Eneo la mgongano linajumuisha mikoa minne nchini Syria. Hata hivyo, Idlib ndiyo iliopewa kipaumbele katika mkutano huu wa Astana. Sababu Idlib ina makundi mengi zaidi kuliko mikoa mingine.

Uturuki, Urusi na Iran waliafikiana kuhusu suala hili, nani atalinda mipaka, na mipaka ya eneo lisilo na migogoro katika Idlib. Kama inavyoonekana katika vyombo vya habari, askari 500 kutoka kila nchi hizo tatu wataweka ngome zao katika vituo vya ukaguzi ili kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Hata hivyo, mpango huu pekee hauwezi kutosha katika kupambana na makundi ya kigaidi.

Urusi, Uturuki, na Iran zinahakikisha kuwa Idlib na vitongoji vinavyoizunguka viko salama . Sio kazi rahisi kwa Uturuki, sababu makundi yanaopigana katika vitongoji vya Idlib yana nguvu na mafunzo ya kijeshi ya kutosha. Kwa hakika, imekuwa muda mrefu tangu kuingia kwa Uturuki katika mkoa huyu ili kuimarisha kuwepo kwa Jeshi la Ukombozi wa Siria katika kanda. Kwa sababu hii, kuna uwezekano mkubwa wa mgogoro kati ya jeshi la ukombozi wa Siria  na makundi mengine, na kisha kati ya jeshi la Uturuki na makundi ya kigaidi na baada ya Uturuki kupeleka askari katika kanda hii. Maandalizi ya kijeshi ya pande zote husika yanathibitisha hili.

Uturuki inatekeleza mkakati na mbinu za hali ya juu ili kukabiliana na makundi makubwa katika Idlib. Hatua ya kwanza ya mkakati huu ni kudhoofisha kundi la HSS, ambalo ni kundi lililoanzishwa chini ya uongozi wa Nusra Front. Jitihada zinafanywa kutenganisha na kubomoa makundi haya ya kigaidi .

Hatua ya pili ya Mkakati wa Uturuki ni uimarishaji wa upinzani wa wastani. Waliotawanyika kutoka Jeshi la Ukombozi wa Siria, wanajaribu kurudi pamoja katika mkoa wa Idlib na kuwa kitu kimoja. Kwa msaada wa Uturuki, vikosi vya Jeshi la Ukombozi wa Siria huko İdlib vilifanikiwa kuja pamoja kwa kiwango kikubwa.

Malengo makuu ya mchakato wa Astana ni kama ifuatavyo:

1) kutenganisha na kubomoa makundi yenye silaha

2) kuondoa wenye msimamo mkali kutoka kwenye makundi yenye msimamo wa wastani

3) kuondoa uhasama kati ya makundi yenye msimamo wa kati na wana siasa

Hivi karibuni, Uturuki itajikuta kwenye hali mbaya katika Idlib. Migogoro huko Idlib inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kuliko shughuli za operesheni ya Fırat Kalkan kwa sababu ya mazingira na hali ya hewa. Kwa sababu hii, kupelekwa kwa jeshi la  Uturuki huko İdlib inaweza kujenga mazingira ya mgogoro ambayo yanaijumuisha Uturuki. Ikiwa Uturuki inaweza kuvumilia migogoro na kupata mafanikio ya kijeshi, Uturuki itaweza kuunda eneo salama kama ilivyokuwa kwenye operesheni ya Fırat Kalkan . Hii itaimarisha mkono wa Uturuki katika mgogoro wa Siria.

Uturuki, ambayo imeendeleza ushirikiano na Syria, Urusi na Iran na ikatekeleza majukumu yake, inaweza kuwa na makubaliano ya kupambana na PKK / YPG. Baada ya Idlib, haishangazi kwamba Uturuki itafungua operesheni nyingine dhidi ya jimbo la Afrin  linalodhibitiwa na PKK / YPG.

 Habari Zinazohusiana