Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Uchambuzi wa matukio

Uturuki imekuwa mgombea wa kujiunga na Umoja wa Ulaya tangu 2005. Harakati za Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya, zimeanza kama fursa kubwa na daraja la matumaini , la kuimarisha uhusiano wa Uturuki na Umoja wa Ulaya, lakini ndoto hizi zimeenda kombo kwa hali na njia ambayo hakuna mtu angeitarajia miaka 12 iliopita.

Uhusiano wa Uturuki na Umoja wa Ulaya kuanzia gazi za chini hadi za kitaifa ziliingia dosari hadi kusitisha uwezekano wa Uturuki kukubaliwa kama mwanachama wa Umoja wa Ulaya. Bila shaka uhusiano wa Uturuki na Umoja wa Ulaya unahitaji kufufuliwa tena. hii inazwezekana endapo pande zote mbili zitakaa pamoja na kutendeana haki kwa kila jambo kwa usawa na heshima.

 

Uturuki imenyanyasika kikweli kuhusu jambo hili la kugombea uwanachama wa Umoja wa Ulaya. Ni wazi matatizo na migogoro tulionayo leo yako mbali sana na mipaka ya Umoja wa Ulaya.Ni dhahari kuwa kuna kukua kwa chuki miongoni mwa raia wa ulaya na ubaguzi wa rangi hasa dhidi ya ulimwengu wa kiislam, na hiyi ndiyo moja wapo wa sababu za kukwamisha harakati za Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Uadui wa baadhi za nchi za Ulaya kwa Uturuki umekuwa moja ya mambo au mizizi ya baadhi ya siasa na wanasiasa wa Ulaya . Jmabo hili limeanza kama jambo la kawaida miaka kumi iliopita, na leo limekuwa jambo la kawaida kwenye siasa ya nchi hizo. Kabla ya kura ya maoni ya kubadilisha katiba ya Uturuki kupigwa, rais wa Uturuki bwana Recep Tayyip Erdogan alijielekeza huko Ulaya kukutana na baadhi ya viongozi wa Ulaya, akiwemo kansela wa Ujeremani, bibi Angela Markel, ili ufunguliwe ukurasa mpya kwenye mahusiano ya Umoja wa Ulaya na Uturuki, na kuwaonya viongozi hawo juu ya uhusiano wao na msaada wanaopatia makundi ya kigaidi yanaopigana na serekali ya Uturuki ikiwemo PKK na FETÖ. Na baada ya kura ya maoni , rais wa Uturuki aliafanya ziara tena huko Brussels, kwenye makao makuu ya Umoja wa Ulaya, lakini jitihada zote hizo za Uturuki hazikufua dafu sababu viongozi wa Ulaya waliendelea kupuuziza na kufumba macho dhidi ya maombi na jitihada za Uturuki.

 

Uturuki ya leo, sio ile Uturuki yam waka 1963 ambapo iliomba kujiunga na shirikisho  la uchumi la Ulaya, wala sio Uturuki yam waka 1999 ilipokubaliwa kama nchi mgombea ya uwanachama wa Umoja wa Ulaya. Uturuki ya leo ni Uturuki imara yenye nguvu kwenye sekta tofauti. Uturuki ya leo ni Uturuki yenye watu mara tatu ya Uturuki ya 1960, na ni Uturuki yenye uchumi uliokuwa kwa kiwango cha asilimia 80 kuanzia kipindi cha mwaka 1963.

Kwa Upande mwingine, Ulaya inapuuza kuwa Ulaya ya leo sio ile Ulaya yam waka 2000. Ulaya ya leo ni Ulaya uliogubikwa namigogoro tele, ikiwemo ubaguzi wa rangi, uchumi kudorora, na usalama mdogo.

Hali ya usalama kutoimarika Ulaya kama zamani, imewafanya waturuki nao kupuuzia na kulegeza Kamba na kuendelea na harakati zake za kugombea uwanachama wa Umoja wa Ulaya.Habari Zinazohusiana