Mafuriko China

Watu watano wameripotiwa kufariki baada ya mvua kali kunyesha katika moja ya miji nchini China.

Mafuriko China

Watu watano wameripotiwa kufariki baada ya mvua kali kunyesha katika moja ya miji nchini China.

Kwa mujibu wa habari,mvua hiyo imenyesha katika eneo la Hubey na kusababisha vifo vya watu watano.

Ripoti zinaonyesha kuwa watu zaidi ya elfu ishirini na sita wamehamishwa makazi yao huku nyumba elfu nane zikiwa zimenguka.

Mali zilizoharibiwa na mafuriko hayo inathamani ya takriban dola milioni 608.

Mwezi uliopita mafuriko kama hayo yaliukumba mji wa Shansi na kusababisha vifo vya watu watano.

 


Tagi: China , mafuriko

Habari Zinazohusiana