"Kama kuna taifa linaloitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jeruselam"

Msimamo wa rais wa Korea-Kaskazini kuhusu kuhusu Jerusalem baada ya uamuzi wa Trump

"Kama kuna taifa linaloitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jeruselam"

 

Rais wa Korea-Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uamuzi wa Trump kutangaza kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel hauna maana yeyote.

Mpango wa Marekani kuamisha ubalozi wake Tel Aviv na kuhamia Jerusalem ni jambo la kukemewa.

Kim Jong Un anapinga uamuzi wa Trump kuhusu jiji la Jerusalem.

Rais wa Korea-Kaskazini amesema kwa kejeli kuwa iwapo kuna taifa linaitwa Israel basi mji wake mkuu uwe Jerusalem.

Kwa mujibu wa kituo cha habari cha Ufaransa cha AFP ni kwamba  msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Korea-Kaskazini amesema kuwa Marekani i natishia amani na utulivu  ulimwenguni .

Ujumbe wake ulimalizia kwa kusema kuwa  Korea-Kaskazini ipo bega kwa bega na wapalestina  na waarabu wanaopigania haki yao.Habari Zinazohusiana