Trump aomba muandishi wa habari afutwe kazi

Rais wa Marekani aomba muandishi wa habari  afutwe kazi baada ya kupeperusha Tweet iliokuwa na ujumbe wa kejeli kwa Trump

Trump aomba muandishi wa habari afutwe kazi

Dave Weigel muandishi wa habari ambwa kufutwa kazi baada ya kupeperusha picha ilikuwa na kejeli kwa rais Trump katika ukurasa wake wa Twitter.

Mwanahabari huyo  alipeperusha picha ambayo ilikuwa ikionesha  jumba la mikutano Pensacola linalopatikana Florida likiwa  wazi wakati ambapo Trump  aliwahutubia  wafuasi wake wiki iliopita.

Mwanahabari huyu aliishindikiza picha yake hiyo na ujumbe wa kejeli uliosema kuwa watu walikuwa wamejaa.

Rais wa Marekani alisema katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Dave Weigel  wa jarida la Washington Post alipeperusha picha isikuwa na ukweli wakati ambapo mkutano ulikuwa bada haujaanza.

Weigel aliomba radhi kwa tukio hilo na kufuta Twit yake hiyo.Habari Zinazohusiana