Miskiti 16 yabomolewa Rakhine Myanmar

Wakaazi katika eneo la Maungdaw wahofia mskiti wa mwisho katika eneo hilo usije kubomolewa

Miskiti 16 yabomolewa Rakhine Myanmar

Wakaazi katika eneo la Maungdaw wahofia mskiti wa mwisho waliosalia usije kubomolewa kama ilivuobomolewa miskiti mingine Rakhine na wabuddha.

Viongozi wa Maungdaw wamesababisha miskiti 16 kubomolewa Rakhine.

Kwa mujbu wa taarifa zilizotolewa na kituo cha runinga cha  "Weekly English News" kwa ushahidi wa wakaazi wa eneo la Maungdaw miskiti 16 imethibitishwa kubomolewa.

Miskiti hiyo imebomolewa kuanzia mwishoni mwa Novemba na mwanzoni mwa Disemba.

Mashahidi wamesema kuwa baada ya majumba yao kubomolewa sasa ni zamu ya nyumba za ibada za waislam kubomolewa.

 Habari Zinazohusiana