Ubalozi wa Urusi nchini Yemen wahamia Saudi Arabia

Urusi yaondoa raia wake na wafanyakazi wake katika ubalozi wake mjini Sanaa nchini Yemen

Ubalozi wa Urusi nchini Yemen wahamia Saudi Arabia

 

Urusi yaondoa wafanya katika ubalozi wake na raia wake wanaopatikana nchini Yemen kufuatia hali ya aslama mdogo unaoripotiwa nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na kituo cha habari cha Saudi Arbaia cha SPA ni kwamba Urusi imeanza kuwaondoa wafanyakazi wake katika ubalozi wake mjini Sanaa.

Raia wa Urusi waliokuwa Yemen wameondoka nchini humo wakitokea uwanja wa ndege wa mjini Sanaa.

Mariya Zaharova, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Urusi amesema kuwa  serikali imechua uamuzi huo kuwaondoa wanadiplomasia wake nchini humo kutokana na hali ya usalama mjini Sanaa.

Msemaji huyo amesema kuwa nusu ya wanadiplomasia wake wataendelea na kazi yao nchini Saudi Arabia.

 Habari Zinazohusiana