Netanyahu afuta kauli yake kuhusu uhamisho wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu

Waziri mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu afuta kauli yake kuhusu uhamisho wa ubalozi wa Marekani  Yerusalemu

Netanyahu afuta kauli yake kuhusu uhamisho wa ubalozi wa Marekani Yerusalemu

 

Waziri mkuu wa Israel Benyamin Netanyahu alifahamisha hapo awali kuwa Marekani itahamisha ubalozi wake ulioko mjini Tel Aviv na kuhamia mjini Jerusalem katika kipindi cha muda mfupi baada ya rais Trump kutangaza kuwa serikali yake inatambua Jerusalem kama mji mkuu wa Israel.

Taarifa zilizotolewa katika tovuti ya Yediot Aharonot  zimemnukuu kiongozi mmoja bila ya kumtaja jina kuwa waziri mkuu wa Israel anatambua vema kuwa ujenzi wa ubalozi mpya unachukuwa muda mrefu.

Trump amekanausha kuwa hakuna mpango wa uhamisho wa ubalozi wa Marekani Jerusalem katika kipindi cha mwaka mmoja huku waziri mkuu wa Israel akiwafahamisha waandishi wa habari  akitokea nchini India kuwa ubalozi wa Marekani utahamisha mwakani.Habari Zinazohusiana