İbrahim Kalın: "Operesheni ya Afrin hailengi jamii ya wakurdi bali magaidi"

Msemaji wa ikulu ya rais Ibrahim Kalın asema kuwa operesheni ya Afrin hailengi jamii ya wakuridi bali magaidi

İbrahim Kalın: "Operesheni ya Afrin hailengi jamii ya wakurdi bali magaidi"

Msemaji wa ikulu ya rais mjini Ankara İbrahim Kaın asema kuwa operesheni ya Afrin nchini Syria hailengi jamii ya wakurdi bali magaidi katika eneo hilo.

Ibrahim Kalın amepinga pia vikali mpango wa serikali ya Marekani kutaka kuunda kikosi mpakani mwa Syria na Uturuki kwa ushirikiano na wanamgambo wa kundi  la kigaidi la PYD ambalo ni kundi linalotambulika kuwa tawi la kundi la kigaidi la PKK nchini Syria.

Msemaji wa rais amefahamisha Alkhamis kuwa  operesheni inayotarajiwa kuendeshwa Afrin hailengi jamii ya wakurdi bali magaidi katika maeneo tofauti  Kaskazini mwa Syria.

Hayo msemaji wa rais aliyazungumza kwa waandishi wa habari baada ya mkutano uliofanyika mjini Istanbul.

Akşzungumzia kuhusu kuundwa kwa kikosi mpakani mwa Uturuki na Syria kwa ushirikiano na wanagambo wa kundi la PYD alifahamisha kuwa Rex Tillerson amekanusha  taarifa kuwa kuna mpango wa kuundwa kikosi hicho mpakani mwa Uturuki.

 Habari Zinazohusiana