Iceland kupiga marufuku ukataji jando

Msuada wa sheria unaopiga marufuku ukataji jando wajadiliwa katika baraza la bunge Iceland

Iceland kupiga marufuku ukataji jando

Msuada wa sheria  kuhusu kupiga marufu ukataji jando wafikishwa katika baraza la bunge na kujadiliwa, iwapo msuada huo utapitishwa, Iceland litakuwa taifa la kwanza barani Ulaya kupiga marufuku ukataji jando.

Jamii ya waislamu na wayahudi  wameonesha kushughulishwa na jambo hilo kwa kuwa imani hizo mbili zinaamuru watoto wa kiume kukatwa jando  kuanzia wanapofikisha umri wa siku 7 na kuendelea.

Msuada huo wa sheria  unapendekeza kuwa  watoto wanaotarajiwa kukatwa jando wawe na sababu za kiafya na uthibitisho wa wataalamu wa afya na yeyote atakae kiuka sheria hiyo anaweza kufungwa zaidi ya miaka 6.

Mtu anaruhusiwa kukatwa jando pindi sheria inapomruhusu. Msuada huo wa sheria unadai kuwa kitendo cha kuwakata jando watoto ni ukiukwaji wa haki za watoto wa kiume ambao bado hawajabalekh.

Jamii ya wayahudi na waislamu  imelaani msauada huo wa sheria  na kusema kuwa ni mfumo mpya wa ubaguzi  kwa waislamu na wayahudi.

Baadhi wa wanasiasa nchini Iceland wanadai kuwa utamaduni wa kukata jando ni utamaduni wa kizamani na uliopitwa na muda.

Iceland ni taifa ambalo lina wakaazi 336 000 wakiwemo waislamu 1 500 na wayahudi 250.Habari Zinazohusiana