Mtazamo

Mgogoro wa Ulaya

Mtazamo

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yıldırım Beyazıt kitengo cha sayansi za siasa Prof. Dr. Kudret BÜLBÜL amefanya tathmini ya mada  ya leo

 

 Mgogoro wa Ulaya

Fikiria kwa muda mfupi,  dunia ingefanya vipi kama Wakristo watano au Wayahudi wangechomwa moto hadi kufa katika nchi unayoishi? (Waislamu 5, ikiwa ni pamoja na watoto 3 wa Kituruki, walikufa mnamo 2 Oktoba 2017 nchini Ufaransa kutokana na moto). Au, ingekuwa  kuna mashambulizi katika masinagogi au makanisa yangechomwa nchini kwetu, ikiwa ingekuaje ?(Kumekuwa na mashambulizi 24 katika misikiti nchini Ujerumani ndani ya robo ya mwisho ya mwaka 2015,Http://gocvakfi.org/almanyada-cami-saldirilari/).

Bila shaka, haifai kuwa na tukio kama hilo katika nchi yoyote. Hata kuuliza swali hili kunaumiza watu. Lakini ukosefu wa usalama katika nchi unayoishi,kuishi katika nchi yako wakati matukio kama hayo ya ukiukaji wa haki na uhuru, vitisho dhidi ya maisha ya watu vinatangazwa hadharani basi hii ni sababu ya kuweka uso wako chini kwa aibu.

Lakini usijali, matukio kama haya hutokea katika nchi za Ulaya, si katika nchi yako. Kutokana na hili,,si wewe wala dunia mnajua kinachoendela.

Ulaya yenye kutengeneza thamani

Ulaya haikuwa hivi hapo awali.Ilikuwa bado ina machungu ya athari za vita vya pili vya dunia na hivyo basi ilikuwa ikihimiza ushirikiano na maelewano na hivyo ndivyo Umoja wa Ulaya ulivyotengenezwa. EU imekuwa na ajenda  ya kupambana na ubaguzi wa rangi,ufashisti,Unazi ,kukuza demokrasia,kulinda haki za binadamu,utawala wa sheria,imeleta maendeleao katika sekta tofauti kama vile uhuru wa kijamii na vilevile uchumi. Ingawa maadili hayo yanapungua,mchango wa EU kwa maadili haya hauwezi kufumbiwa macho.

Japokuwa George Friedman, alizungumza kuhusu "Mgogoro wa Ulaya" kati ya 1945 na 1991,hakuzungumzia Ulaya, bali aliongelea Marekani pamoja na Urusi kuleta amani barani Ulaya.Mimi sikubaliani na hilo.Ulaya ya zamani si Ulaya ya hivi sasa.Jinsi siku zinavyoendelea maadili ya Umoja wa Ulaya yanazidi kupungua,raia wa kigeni wanapigwa vita,uadui dhidi ya wahamiaji unaongezeka,Vyama vya Fascist na Nazist vinaongeza kura zao.

Vyama vya Wabaguzi wa rangi sasa ni washirika wenye nguvu. Wakati viongozi wenye busara wanavyozidi kudidimia, viongozi wasio na busara wanaongezeka siku hadi siku. Mashambulizi tofauti dhidi ya watu na ibada yao hayazungumziwi hata katika vyombo vya habari.Uchunguzi na utafiti umeonyesha kuwa wahamiaji wanapata taabu zaidi na kutengwa jinsi siku zinavyoendelea.

Vyama vya kisiasa badala ya kuzungumzia ajenda zitakazoifanya na kuisaidia nchi yao kuwa nchi bora zaidi,vimekaa vikijadili mbinu za kuondokana na wahamiaji.Kwa mfano Austria ambapo wahamiaji wamefanywa kuwa ni tishio kwa taifa.Ni jambo la kusikitisha kwani hawawezi kufikia hata asilimia moja ya wahamiaji walio nchini Uturuki.

Kupotea kwa busara

Nchi zinaweza kuingia katika migogoro hiyo mara kwa mara. Katika hali hiyo, taasisi za serikali na viongozi  huendeleza sera za busara zaidi ili kuzuia kuongezeka kwa mgogoro huo. Ikiwezekana, wataiondoa nchi yao kutoka katika mgogoro huo.

Lakini tukitizama wanavyowafanyia wahamiaji, Waislamu,wanavyoishutumu Uturuki kwa shutuma zisizoeleweka tunaona kabisa kuna tatizo la akili barani Ulaya.

Tunanaona kabisa kuwa Ulaya imepoteza uwazi na mwelekeo wake. Ulaya imekuwa dhaifu.

Usitupe lawama za matatizo ya Ulaya kwa wahamiaji

Huu ni mgogoro wa Ulaya. Wahamiaji, Waislamu na Waturuki wamekuwa wakiishi Ulaya kwa muda mrefu. Kwa  sasa idadi ya wahamiaji bbarani humo inapungua kwa kasi.Wahamiaji hawajabadili mbinu na njia zao za kuishi.Ulaya imekuwa ikitumia lugha mbaya na ubaguzi dhidi ya wahamiaji.

Hii ina maanisha kuwa tatizo halitoki kwa wahamiaji bali tatizo linatoka kwa Ulaya yenyewe ambayo ina badilisha maadili yake siku hadi siku.Tukitizama msingi wa mgogoro huo tutaona kuwa umesababishwa na matatizo katika uchumi,mapungufu katika utandawazi na kutoijua vizuri historia ya Ulaya.

Ulaya ilisumbuliwa na mambo kama haya kabla ya vita vya pil vya dunia. Ulaya, ambayo haikuweza kuona matatizo yake yenyewe,ilianza kurusha lawama zote kwa Wayahudi bila kutambua kuwa tatizo linatoka kwao wenyewe.Ni wazi kuwa  mgogoro wa Ulaya na vita vya pili vya dunia havikusababishwa na Wayahudi.Vitendo vya Ulaya  viliifanya dunia nzima ihangaike kutokana na kutokea kwa WWII.

Hivi  leo Ulaya inajijadili yenyewe na  maisha yake ya baadaye kwa kupitia uhuru wa Waislamu na wahamiaji.Mashambulizi dhidi ya wahamiaji na waislamu yanatokana na ujinga .Viongozi Ulaya wanapashwa kuwa makini na kutorudia makosa waliokuwa wakiyafanya kabla ya vita vya pili vya dunia.Inapashwa kufanya hivyo ili kuzuia kujirudia kwa makosa na historia.Ili kufanya hivyo inabidi kwanza itambue kuwa Wahamiaji,Waislamu wala Waturuki  si sababu kuu ya matatizo yao.Sina matumaini kama Ulaya itaweza kuutatua mgogoro wake yenyewe.Ulaya kuutatua mgogoro wake yenyewe,hio ni mada nyingine kabisa.

Kutoka katika chuo kikuu cha Ankara Yildirim Beyazit kitengo cha Sayansi za Siasa Dr. Kudret BÜLBÜL alipendekeza tathmini ya suala hilo

 

 Habari Zinazohusiana