Pesa zilizobaki katika  bajeti ya mwaka 2017 nchini Singapore wapewa raia

Raia wenye umri wa miaka zaidi ya 21 wapewa  pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 nchini Singapore

Pesa zilizobaki katika  bajeti ya mwaka 2017 nchini Singapore wapewa raia

Serikali ya Singapore imefahamisha kutoa pesa zilizobaki katika bajeti ya mwaka 2017 kwa raia wake wote  wenye umri wa zaidi ya miaka 21.

Raia wote wenye umri wa zaidi ya miak 21  wataongezewa kiwango cha dola 100 hadi 300 katika miishahara yao.

Bajeti iliopangwa na kutolewa kwa mwaka 2017 ilitumiwa na kiwango kikubwa cha pesa hakikutumika.

Waziri wa fedha wa Singapore Heng Swee Keat amesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa  baada ya kuona kuwa bajeti ilikuwa kubwa.

Waziri wa fedha amesema kwa serikali ya Singapore inatumikia raia wake na kuwa na lengo la maendelea kwa kila raia wake.

Ikumbukwe kuwa Singapore ilitoa kiwango cha dola 100 hadi 800 kwa raia wake mwaka 2011.Habari Zinazohusiana