Usiku wa Miraj

Waislamu wanatarajia kusherehekea usiku wa Miraj

Usiku wa Miraj

Kwa mujibu wa dini ya kiislamu usiku wa Miraj ni usiku ambao Mtume Muhammad(SAW) alialikwa na Mwenyezi Mungu na kupelekwa katika mbingu saba na malaika Jibril.

Mtume Muhammad(SAW) alipelekwa kutoka msikiti wa Masjid al-Haram hadi Masjid al-Aqsa na baadae kupelekwa mbinguni.

Usiku huo ni usiku muhimu kwa waislamu kwani Mwenyezi Mungu alimpa Mtume Muhammad(SAW) amri kumi na mbili muhimu.

Quran itakuwa ikisomwa katika misikiti tofauti nchini Uturuki katika kuupokea usiku huo.


Tagi: Miraj , Usiku

Habari Zinazohusiana