Umoja wa Mataifa na unyanyasaji wa kingono Syria
Umoja wa Mtaifa walituhumu kundi la PKK/PYD kuhusika na unyanyasaji wa kingono nchini Syria

Ripoti ya Umoja wa Mataifa yatuhumu wanamgambo wa kundi la PKK/PYD kuwanyanyasa kingono wanawake nchini syria.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa imetuhumu kundi la wanamgambo wa PKK/PYD kuhusika na mtendo ya unyanyasaji nchini Syria.
Ripoti hiyo imelituhumu kundi hilo kuhusika na matendo ya unyanyasaji wa kingono kwa wanawake katika mapigano na harakati zake.
Katika mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mtaifa kuhusu unyanyasaji wa kingono katika mapigano, muakilishi wa Uturuki Güven B amezungumzia kuhusu unyanyasaji wa kingono wanaotendewa wanawake nchini Syria na wanamgambo wa kundi la kigaidi la PKK/PYD na wanamgambo wa kundi la Daesh.
Ripoti hiyo imetuhumu kundi hilo kuendesha vitendo vya kikatili kwa raia. Wanaume kuteswa hadi kufikia kuchomo moto katika sehem zao za siri.
Vile vile muakilishi wa Uturuki amezunguzi kuhusu jamii ya Rohingya ambayo pia ipo katika madhila kama hayo.