Mpaka pekee  wa kibiashara Ukanda wa Gaza wafungwa na Israel

Israel yafunga mpaka pekee wa kibiashara bain aya  Ukanda wa Gaza na Israel

Mpaka pekee  wa kibiashara Ukanda wa Gaza wafungwa na Israel

Mkurugenzi wa baraza la ruhusa kuhusu bidhaa Ukanda wa Gaza Raed Futuh  amesema kuwa  mkapa pekee wa kibiashara katia ya Ukanda wa Gaza  na Israel umefungwa na mamlaka ya Israel.

Taarifa zinafahamisha kuwa mpaka huo umefungwa bşla ya kufahamishwa ni lini utafunguliwa. Raed amesema kuwa  mpaka huo utafunguliwa  wakati kutakapotolewa  amri kutoka  serikalini.

Madawa pekee ikiwa mahitaji kwa wagonjwa ndio yatakayoruhusiwa kupita katika mpaka huo baina ya Israel na Ukanda wa Gaza.

Chama cha Hamas kimekemea uamuzi  ambao kwa kujibu wake lengo lake ni kuathiri maisha ya kila siku ya wapalestina  na  kukemea pia ukimya wa jumuiya ya kimataifa inayofumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu  Ukanda wa Gaza na katika maeneo ya wapalestina.

Misri nayo kwa upande wake imefahamisha kufunga   kituo cha mpaka cha  Rafah.

Kituo hicho cha mpakani baina ya Ukanda wa Gaza na Misri huwa kikifungwa mara kwa mara tangu kupinduliwa kwa rais Mohammed Morsi Julai 3 mwaka 2013.Habari Zinazohusiana