"Marekani haitoshinda katika vita vya kiuchumi dhidi ya Uturuki"

Balozi wa zamani wa Marekani mjini Ankara nchini Uturuki asema kuwa Marekani haitoshinda vita vya kşuchumi dhidi ya Uturuki

"Marekani haitoshinda katika vita vya kiuchumi dhidi ya Uturuki"

Ross Wilson, balozi wa zamani wa Marekani mjini Ankara nchini Uturuki asema kuwa vita vya kiuchumi vya Narekani dhidi ya Uturuki Marekani haitoshinda.

Balozi huyo wa zamani wa Marekani ameendelea akisema kuwa  soko la kimataifa  pia litaathirika.

Katika mahojiano aliofanya katika kituo cha  FOX TV Ross Wilson amesema kuwa  vikwazo dhidi  ya Uturuki vitakuwa na  madhara dhidi ya Marekani bila ya kuweka kando  madhara katika soko la kimataifa.

Ross Wilson  amezungumzia kuhusu  madhara ya  vikwazo  dhidi ya Uturuki. Ushirikiano kati ya Uturuki na Marekani  ulikuwa ushirikiano  muhimu kwa muda mrefu.

Madhara ya vikwazo hivyo yataathiri pia soko la kimataifa.

Ross Wilson  ameitahadharisha Marekani na madhara yatakayosababishwa na  vikwazo vya Marekani dhidi ya Uturuki na kuitolea wito kurejea katika uamuzi wake.

 

 

 Habari Zinazohusiana