Milango ya msikiti wa Al Aqsa yafunguliwa

Mamlaka ya Israel imefungua kwa mara nyingine milango ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa.

Milango ya msikiti wa Al Aqsa yafunguliwa

Mamlaka ya Israel imefungua kwa mara nyingine milango ya msikiti mtukufu wa Al Aqsa.

Milango ya msikiti huo ilifungwa kwa muda wa siku moja.

Kufungwa kwa milango ya msikiti huo kulifanyika baada ya polisi wa Israel kumpiga risasi na kumuua raia wa Israel mwenye asili ya kiarabu kwa shutuma za kuwa alikuwa na nia ya kumchoma kisu afisa polisi.

Kiongozi wa msikiti huo Sheik Omar Kiswani amekiambia kituo cha habari cha Anadolu kuwa sasa polisi wa Israel wameshaona ni jambo la kawaida kufunga milango ya msikiti wa Al Aqsa kila mara.

Polisi wa Israel walifunga milango ya msikiti huo mara mbili mwezi uliopita.Habari Zinazohusiana