Uturuki na Ufaransa zajadili vikwazo vya Marekani

Waziri wa fedha wa Uturuki Berat Albayrak amefanya mazungumzo na waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire.

Uturuki na Ufaransa zajadili vikwazo vya Marekani

Waziri wa fedha wa Uturuki Berat Albayrak amefanya mazungumzo na waziri wa fedha wa Ufaransa Bruno Le Maire.

Mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao yamegusia tathmini ya vikwazo vya kiucuhumi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Uturuki.

Nchi hizo mbili zimejadili jinsi ya kushirikiana kiuchumi dhidi ya vikwazo vya Marekani.

Waziri Albayrak ametoa shukrani kwa Emmanuel Macron na Bruno Le Maire kwa kuiunga mkono Uturuki.

Albayrak na LeMaire wanatarajia kukutana mjini Paris ifikapo 27 Agosti.Habari Zinazohusiana