Uturuki yakemea taarifa zilizotolewa na jarida la "The New York Times " dhidi ya Uturuki

Msemaji wa ikulu mjini Ankara akemea taarifa zilizotolewa na jarida la "The New York Times" la Marekani kuhusu kundi la kigaidi la PKK

Uturuki yakemea taarifa  zilizotolewa na jarida la "The New York Times " dhidi ya Uturuki

Msemaji wa ikulu Ibrahim Kalın mjini Ankara akemea taarifa zilizotolewa na jarida la "The New York Times" la Marekani kuhusu kundi la kigaidi la PKK.

Ibrahim Kalın amekemea taarifa iliochapishwa na jarido hilo ambayo ilikuwa ikizungumzia kundi la kigaidi la PKK  na kulikebehi taifa la Uturuki.

Kwa mujibu wa msemaji wa ikulu mjini Ankara jarida hilo la Marekani  limejaribu kutetea kundi hilo na kuliondoa miongoni mwa makundi ya kigaidi.

Ibrahim Kalın amekemea jarida hilo katika ujumbe waliotoa katika ukurasa wake wa Twitter.

Msemaji wa  serikali ya Uturuki amekemea jarida hilo kwa kusema kuwa iwapo watu watafuata mtazamo huo basi Ben Laden, Milosevic na Mladic ambao wanafahamika kwa matendo yao watakuwa ni mashujaa.

 Habari Zinazohusiana