Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa Michezo

Karibu tena katika kipindi chetu cha ulimwengu wa michezo, tukiwa tayari kukuhabarisha juu ya yale yaliyojiri katika viwanja mbalimbali vya michezo duniani.

Awali ya yote tutaanzia kwenye fainali za mashindano ya wazi ya mchezo wa Tenis Marekani. Rafael Nadal aliibuka bingwa wa mashindano hayo ya 16 ya Grand Slam. Kwa ushindi huo mwanana, Nadal anakuwa ndio mchezaji nambari moja kwa ubora wa mchezo huo duniani. Nadal alishinda taji hilo baada ya kumgaragaza mpinzani wake kwa seti tatu mtungi kwa matokeo ya 6-3/6-3/6-4. 

Kiukweli, mashindano haya yameshuhudia mechi za kuvutia sana msimu huu. Awali ya yote, kukosekana kwa nyota wakubwa wengi kama vile Murray, Djokovic, Wawrinka, Raonic na Shikori kuliwapa uwezo nyota wadogo kung'aa. Mfano mzuri ni Rublev mwenye umri wa miaka 19, ambaye alifanikiwa kutinga robo fainali ya mashindano haya kabla ya kutolewa na Nadal. Mchezaji nambari 24 kwa ubora, Del Potro alimshinda nyota nambari tatu, Federer katika hatua ya robo fainali. Mashabiki wengi walitaraji kushuhudia mpambano mkali wa nusu fainali baina ya Federer na Nadal, Lakini Potro alimwondosha Federer katika hatua ya robo fainali. Mchezaji namba 28 kwa ubora, Kavin Anderson alipambana na mchezaji namba 12 Carreno Busto na kumtoa katika nusu fainali. Japokua Nadal ameibuka bingwa, wapenzi wengi wa tenisi hawakufurahishwa na kitendo cha fainali kuisha kwa seti tatu tu. 

 

Mambo hayakuwa haba kwa upande wa wanawake pia. Fainali ya wanawake ilichezwa baina ya mchezaji nambari 83 kwa ubora, Sioane Stephans dhidi ya nambari 15 kwa ubora, Madison Keys. Wote

hawa ni Wamarekani.  Stefans aliibuka mshindi dhidi ya Keys kwa kumshinda set 2-0 za 6-3 na 6-3 na kutwaa taji hilo ambalo ameshiriki kwa Mara ya kwanza. 

Kama ilivyo kwa upande wa wanaume, upande wa wanawake pia umeshuhudia ujio wa majina mapya. Mfano  mchezaji nambari moja kwa upande wa wanawake Pliskova aliondoshwa katika mashindano hayo na Wenderweghe katika hatua ya robo fainali, wakati nyota nambari mbili, Halep alibwagwa na Sharapova katika hatua ya kwanza ya mashindano hayo. Wengine waliotolewa ni pamoja na nyota nambari tatu, Maguruza katika hatua ya 4, nyota nambari tano, Wozniacki katika hatua ya 2, nyota nambari nne, Svitolina katika hatua ya nne na Kerber katika hatua ya pili ya mashindano hayo. Ulimwengu wa tenisi umeanza kutawaliwa na majina mapya. 

 

Kwa baadhi ya michezo, mchezaji akifika miaka 32, huhesabika kuwa wakati wake umefikia ukingoni. Lakini kula mlo kamili kwa kufuata maelekezo, kuishi kwa kufuata kanuni za afya, kujituma sana, kuwa na nidhamu, kujiamini na kuwa na malengo thabiti huweza kuondoa dhana hii. Mfano mzuri wa hili ni mwendesha baiskeli maarufu, Chris Frome. Licha ya kuwa na miaka 32, bado Frome ana uwezo mkubwa wa kukanyaga pedari za baiskeli. Baada ya kushinda mashindano ya baiskeli ya Ufaransa kwa mara tatu mfululizo, Frome sasa ameibuka kidedea katika mashindano ya baiskeli ya Uhispania, na kuwa mchezaji wa pili katika historia kufanikiwa kushinda mataji mawili ndani ya mwaka mmoja. Baada ya kukamilisha mashindano hayo yaliyokua na duru 21 na kudumu kwa majuma matatu, Frome ambaye aliibuka kidedea alieleza kuwa, alikusudia kuwa mshindi wa mashindano hayo. Frome alionesha furaha ya juu na kujisikia fahari kwa kushinda mashindano hayo ya Uhispania. Mwanamichezo wa kwanza kushinda mataji hayo mawili alikua ni Bernard Hinault wa mwaka 1978. 

Wakati huohuo, mwenyesha baiskeli maarufu wa Uhispania, Alberto Cantador aliwaaga mashabiki wake walipoenda katika duru ya Madrid. Cantador amestaafu mashindano hayo akiwa na miaka 34.

 

Tukielekeza macho yetu katika mashindano ya kuendesha magari, ya MotoGP, Mhispania Marc Marquez ameibuka mshindi wa hatua ya 13. Hatua ya 13 iliyokua na urefu wa kilomita 4.2 na mizunguko 28 ilifanyika katika eneo la kimataifa la mashindano la Misano Marco Simonelli. Hii ni mara ya nne kwa Marquez kushika nafasi ya kwanza katika msimu huu na mara ya 33 katika maisha yake ya mashindano hayo. Waitaliano, Danilo Petrucci na Andrea Dovizioso walifuatia kwa kushika nafasi ya pili na tatu. Kwa kushinda hatua hii ya 13, Marc zmarquez sasa amemfikia idadi ya alama Andrea Dovizioso na wote wanawania nafasi ya kwanza ya mashindano hayo wakiwa na alama 199.  Nafasi ya tatu kwa ujumla inashikwa ja Maverick Vinales mwenye alama 183, Valentino Vinales nafasi ya nne kwa alama 157 huku Dani Pedrorso akishika nafasi ya tano kwa alama 150..

Hatua ya 14 ya mashindano ya MotoGP inatarajiwa kufanyika huko Aragon Grand Prixi mnamo tarehe 24 Septemba.

 

Mashindano ya mpira wa kikapu barani Ulaya yanakaribia mwishoni. Mashindano hayo yaliyoanza kwa  kuwa na makundi 4 yenye timu sitasita, sasa yamefikia fainali ambayo itachezwa siku ya Jumapili ya tarehe 17 Septemba. Swali gumu ni nani atatinga fainali hizo, timu zilizopewa nafasi kubwa ya kushinda, au itakua ni mshtukizo?. 

 

Ulimwengu wa michezo asla hauishi.....Habari Zinazohusiana