Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo

Ulimwengu wa michezo 

Siku zinazidi kusogea mbele na misimu ya hali ya hewa inabadilika.Wapenzi wa michezo ya mpira wa kikapu na kadhalika wanazidi kufurahia na kushangilia huku michezo ya wakati wa baridi yani winter ipo njiani kuanza.

 

Katika mashindano ya mpira wa wavu ya wanawake ,timu ya Serbia imeweza kuishinda timu ya Holland kwa 3-1 na kujipatia ubingwa wa Ulaya katika mechi iliyochezwa mjini Baku.

Uturuki iliweza kuishinda Azerbaijan kwa 3-1 katika nusu fainali na kujichukulia nafasi ya tatu.

 

Mashindano ya Formula 1 yanafikia ukingoni.Ni mashindano matano tu yamebaki kuumalizia msimu huu.Katika mashindano yaliyofanyika Malaysia mchezaji Max Verstappen amekuwa wa kwanza msimu huu.Mashindano hayo yaliyofanyika mjini Selagor yalifanywa ndani ya mita 543 kwa raundi 56.Verstappen alimaliza kwa daraja 1.30.01.290.Hapo awali aliyekuwa akiogoza katika mashindano hayo alikuwa ni Lewis Hamiltonu.

Katika raundi ya 15 Lewis Hamiltonu alikuwa wa pili,Daniel Ricciardo wa tatu.

Katika mashindano ya Malaysia mchezaji Lewis Hamilton alimaliza kwa pointi 281.Sebastian Vettel 247 na katika nafasi ya tatu Valtteri Bottas pointi 222.Mashindano ya kumi na sita yatafanyika Oktoba 6 Grand Prixi Japan.

 

Kila mchezo una hatari zake.

Mashindano ya kuendesha pikipiki ni kati ya mashindano hatari kabisa kwani unaweza kupata ulemavu wakati wowote.Tumtizame Kenan Sofuoğlu.Mchezaji huyu alipata majeraha kadhaa wakati wa mashindano.Kenan hatoweza kushiriki kwenye baadhi ya mechi kutokana na majeraha hayo.Sofoğlu atahitaji kupona kidogo ili kuweza kushiriki katika mashindano nchini Uhispania wiki lijalo.

Kutokana na majeraha aliyokumbana nayo Kenan,ubingwa wa Supersport umechukuliwa na mchezaji Niki Tuuli.

Mashindano ya kumi yatafanyika Paris katika uwanja wa Nevers Magny-Cours.

Katika mashindano ya mita 411 Niki Tuuli alikuwa wa kwanza,Federico Caricasulo wa pili,Partick Jakobseb wa tatu .Nafasi ya Kenan Sofoğlu kwa sasa imechukuliwa na Lucas Mahias.Mahias ameweza kujiongezea pointi zake mpaka 154 huku Kenan Sofoğlu alikuwa na pointi 145.Sheridan Morais 122,Jules Cluzel 115 na katika nafasi ya tano Patrick Jakobsen pointi 95.

Katika mashindano ya Motor Spor mchezaji mwingine kutoka Uturuki Toprak Razgatlıoğlu ameumia wakati wa mazoezi.Mchezaji huyo amepata majeraha ya goti na hivyo basi daktari amemkataza kushiriki katika mashindano yoyote kwa sasa.Kwa kawaida Razgatlıoğlu alimaliza wa pili kwa pointi nane katika mashindano ya Ulaya ya 1000 Superstock.

 

 

Tukitizama mchezaji maarufu wa Golf Tiger Woods.Mchezaji huyu alikuwa akijulikana sana kwa kupata medali nyingi na kupata ubingwa mara 14.Kwa sasa haoni muelekeo wake hasa baada ya kufanyiwa upasuaji.

 

Nchi zilizokutwa na makosa ya wachezaji wake kutumia dawa za kuongeza nguvu katika mashindano ya olimpiki 2008-2012 zimepeww adhabu ya kutoshiriki mashindano ya kimataifa kwa mwaka mmoja.Ni takriban nchi nane zimekutwa na makosa hayo.

 

Mashindano ya mpira wa miguu ya walemavu ya Ulaya yameanza rasmi mjini Istanbul.Mashindano hayo yamegawanya timu katika makundi yafuatayo:

Kundi A Uturuki,Uhispania,Georgia

Kundi B Poland,Ufaransa,Italia na Ubelgiji

Kundi C Urusi,Uingereza,Ireland,Ugiriki 

 

Ulimwengu wa michezo daima hauna mwisho Habari Zinazohusiana