Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Adriano aonesha nia yake ya kurudi uwanjani

Mchezaji wa kimataifa wa Brazili Adriano alisema kwenye kipindi cha  televisheni Alhamisi kuwa anataka kurudi uwanjani ifikapo mwaka 2018

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil Adriano aonesha nia yake ya kurudi uwanjani

 

Mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Brazili Adriano alisema kwenye kipindi cha  televisheni Alhamisi kuwa anataka kurudi uwanjani ifikapo mwaka 2018.

Mchezaji huyo wa zamani wa Inter Milan, Adriano, ameweka wazi nia yake ya kucheza mpira wa miguu tena mwaka 2018. 

Adriano alisema:  "Nataka kurudi uwanjani  hivi karibuni . Najihisi vizuri, sijaacha mazoezi. Ninatarajia kupambana na changamoto hii mpya. "  Adriano alisema hayo wakati wa kipindi na  kituo cha Brazili Globo kwenye programu ya " Conversa com Bial ".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 alishinda mataji  manne ya Italia (Serie A), alipokuwa akiichezea  Inter Milan (2006, 2007, 2008 na 2009).

Akiwa pamoja na Ronaldo walitengeneza safu nzuri  ya washambuliaji, na hao wawili wakachangia timu ya taifa ya Brazil, Seleção , kutwaa kombe la Copa América (2004) na Kombe la Confederations (2005).Habari Zinazohusiana