Watalii milioni 2,5 kutoka Iran nchini Uturuki

Shirika la kupokea watalii la Uturuki latoa idadi ya watalii kutoka Iran waliotembelea Uturuki mwaka 2017

Watalii milioni 2,5 kutoka Iran nchini Uturuki


Shirika la kupokea wageni la Uturuki (TÜROB) limetoa ripoti yake ya mwaka 2017 na kufahamisha kuwa watalii milioni 2,5 kutoka Iran walitembelea Uturuki.

Takwimu za mwaka 2016 zilizotolewa na wizara ya utali ya Uturuki zimeonesha kuwa watalii milioni 1,6 ndio waliotembelea nchini Uturuki.

Takwimu hizo zimeonesha kuwa  watalii wengi kutoka Iran  katika kipindi cha mapumziko huvutiwa na Uturuki.

Kiwango cha watalii kutoka Iran mwaka 2018 kinatarajiwa kuongezeka mwezi Machi.


Tagi: Iran , utalii , Uturuki

Habari Zinazohusiana