Quincy Jones amtuhumu Michael Jackson kuiba wimbo "Billie Jean"

Mtaarishaji maarufu wa muziki Quincy Jones amtuhumu Michael Jackson kuimba nyimbo zake nyingi ambazo zilimpa umaarufu mkubwa

Quincy Jones amtuhumu Michael Jackson kuiba wimbo "Billie Jean"

 

Mtaarishaji maarufu wa muziki Quşncy Jones amtuhumu mfalme wa muzşkş wa Pop Michael Jackson  kuiba nyimbo zake kadhaa ambazo zilimpa umaarufu ukiwemo wimbo "Billie Jean".

Quincy Jones amesema kuwa hakuwa na haja na kuzungumza hadharani ila Michael Jackson aliiba kazi nyingi .

Quincy Jones ambae sasa ana umri wa miaka 84 alishiriki katika utaarishaji wa albamu ya "Thriller" na "Bad" ambazo zilimpa umaarufu mkubwa Michael Jackson. Jones amesema kuwa Michael Jackson aliiba nyimbo nyingi.

Quincy aliyazungumza hayo katika mahojiano aliofanya katika tovuti ya Vulture Jumanne.

Mtaarishaji huyo wa muziki amezungumzia wimbo wa "Billie Jean" na kumtuhumu Michael Jackson  kuiba wimbo wa "State of Independence" wa Donna Summer uliotaariashwa na Quincy Jones.

Jones katika mahojiano aliofanya katika jarida la GQ alisema kuwa alipewa matibabu  nchini Uswidi ambayo yatampa uwezo wa kuishi hadi atakapofikisha miaka 110.

 

 Habari Zinazohusiana