Raia wasusia kufanya ununuzi wa matunda nchini Pakistan

Raia nchini Pakistan wasusia kununua matunda kufuatia kupanda kwa bei mwezi mtukufu wa Ramadhan

Raia wasusia kufanya ununuzi wa matunda nchini Pakistan

Kampeni kupitia mitandao ya kijamii yaanzishwa kwa lengo la kususia  ununuzi wa matunda kwa siku tatu mfululizo nchini Pakistan .

Raia nchini humo wamelalamika kwamba bei za matunda zimepanda kupita kiasi hasa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Raia kadhaa nchini Pakistan wamekuwa wakishawishana kuunga mkono kampeni hiyo dhidi ya wauzaji ili kuwalazimu kushusha bei hizo za matunda .

Wanunuzi wana uhakika kwamba ususaji huo utafanya kazi kwani matunda hayo yataanza kuharibika na kupelekea hasara kuu kwa wauzaji hivyo basi kupelekea kushukishwa kwa bei hizo.

Ujumbe wa kampeni hiyo umekuwa ukismabzwa katika mitandao ya Facebook,Whatsup na mengineyo na kutoa wito kuanzishwa kwa harakati hiyo kwanzia Juni 2 hadi Juni 4.

 

 Habari Zinazohusiana