Uturuki kushirikiana na Boeing katika utengenezaji wa ndege

Waziri wa uchumi wa Uturuki, Nihat Zeybekci, alisema kuwa Uturuki ina mpango wa kutengeneza  Boeing za kituruki

Uturuki kushirikiana na Boeing katika utengenezaji wa ndege

 

Waziri wa uchumi wa Uturuki, Nihat Zeybekci, alisema kuwa Uturuki ina mpango wa kutengeneza  Boeing za kituruki .

Nihat Zeybekci amesema  kuwa Uturuki nia yake sio kununua ndege za Boeing bali kutengeneza vifaa vyake.

Zeybekci aliyafahamisha hayo akiwa katika mkutano na viongozi wa Boeing mjini  New York.

Alionesha nia ya Uturuki ya kutaka  kushirikiana na Boeing na kufanya makampuni ya Uturuki kuwa mshirika wa Boeing katika sekta ya utengeneza wa vifaa vya ndege. Habari Zinazohusiana