İphone X yatolewa kasoro na Marekani

Marekani imeitoa kasoro simu mpya ya Iphone X  na kusema kuwa ufunguaji wa simu hiyo kwa kutumia uso pekee sio sahihi hasa kwa mapacha na watoto wa chini ya umri wa miaka 13.

Kwa mujibu wa habari,kitengo cha teknolojia nchini Marekani kimeitaka simu hiyo kutengeneza aina nyingine ya password na sio sura peke yake.

Vilevile kitengo hicho kimesema kuwa baadhi ya sura za watoto zinakuwa hazijakua na kutambulika vizuri na kutokana na sababu hiyo itakuwa ni vigumu kwao kutumia iphone X.

Ripoti zilizotolewa na Marekani zimeonyesha kuwa mapacha au watu wanaofanana watapata shida katika utumiaji wa simu hiyo.

Mwezi uliopita kampuni ya İphone ilikubali kasoro ya tatizo la sauti kwenye İPHONE 8 na kuahidi kulishughulikia.

 Habari Zinazohusiana