Tume ya wafanyabiashara kutoka Uturuki yawasili nchini Ethiopia

Tume ya wafanyabiashara kutoka Uturuki yawasili nchini Ethiopia kwa lengo la kusaini mikataba ya ushirikiano

Tume ya wafanyabiashara kutoka Uturuki yawasili nchini Ethiopia

Balozi wa Uturuki nchini Ethiopia amesema kuwa lengo la Uturuki ni  kufufua ushirikiano na kuimarisha uchumi kupitia sekta ya biashara. Tume ya wafanyabiashara kutoka Uturuki iliowasili mjini Addis Ababa imetoa wito Ijumaa wa kudumisha soko huria bain aya Uturuki na Ethiopia kwa lengo la kuimarisha  uchumi.

Tume hiyo ya wafanya biashara kutoka Uturuki ilitembelea chumba cha biashara cha Ethiopia ECCSA mjini Addis Ababa na kuzungumzia ushirikiano katika sekta ya biashara bain aya Uturuki na Ethiopia.

Ushirikiano huo katika sekta ya biashara utahusu pia sekta ya  mavazi, vifaa vya kielektoniki na madawa.

 Habari Zinazohusiana