Katibu mkuu wa NATO katika ziara yake rasmi nchini Uturuki

Jens Stoltenberg, katibu mkuu wa NATO katika ziğara yake rasmi nchini Uturuki

Katibu mkuu wa NATO katika ziara  yake rasmi nchini Uturuki

Katibu mkuu wa jeshi la kujihami la Magharibi NATO Jens Stoltenberg amewasili mjini Ankara nchini Uturuki katika ziara yake ya siku kadhaa ambapo anatarajiwa kukutana na viongozi tofauti.
Stoltenberg amepokelewa na waziri wa ulinzi wa Uturuki Nuretin Canikli  mjini Ankara.

Canikli ametoa shukrani kwa katibu mkuu wa NATO kwa ushirikiano katika mapambano dhidi ya  ugaidi.
Katibu mkuu wa NATO ametoa salam kwa wanajeshi walihudhuria katika mapokezi yake mjini Ankara.

Stoltenberg amekutana na kufanya mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu.

Mapambano dhidi ya ugaidi  na makundi ya kigaidi kama PKK/KCK/PYD na kundi la Daesh yamezungumziwa .
Katibu mkuu wa NATO amepokelewa pia na raisErdoğan ikulu mjini Ankara.Habari Zinazohusiana