Arda Turan huenda akihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 12 kwa kosa la kupigana na mwanamuziki

Nyota wa kabumbu  Arda Turan huenda akahukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 12 kwa kosa la kupigana na  mwanamuziki mjini Istanbul

Arda Turan huenda akihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 12 kwa kosa la kupigana na mwanamuziki

Arda Turan, nyota wa kimataifa ya kabumbu  na kiungo wa zamani wa Barcelona  na Atletico di Madrid  huenda akahukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka 12 na nusu kwa kosa la kupigana na mwanamuziki  wa kituruki Berkay Sahin mjini Istanbul.

Muandesha mashtaka mkuu wa Istanbul apendekeza adhabu ya kşungo cha miaka 12   kwa Arda Turan  kwa kutuhumiwa unyanyasaji wa kijinsia na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Arda alikutana na Berkay usiku wa Oktoba 10 katika  ukumbi wa muziki mjini Istanbul na baada ya muda kuzuka ugomvi.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na mashuhuda wa tukio hilo kwamba mke wa Berkay alidai kuwa amenyanyaswa kijinsia na Turan.

Berkay alipelekwa hospitali kufuatia ghasia zilizozuka na baada ya muda Arda aliwasili katika hospitali hiyo kumueleza Berkay kuwa hakuwa anatambua kuwa mwanamke huyo alikuwa ni mke wake huku akiwa na silaha.

Tukio hilo linafuatiliwa kwa ukaribu.Habari Zinazohusiana