Uturuki kuweka wazi sakata zima kuhusu tukio la Khashoggi

Uturuki yaahidi kuweka kila kitu wazi bila kuficha chochote kuhusu sakata zima la mauaji ya Kashogghi

cemal.JPG
Ömer Çelik.jpg

Jumamosi hii msemaji wa chama tawala cha Uturuki, AK party, Ömer Çelik asema Uturuki itaweka wazi kila kitu kuhusiana na mauaji ya Kashoggi baada ya uchunguzi na itafichua kila kitu kwamba mtu yeyote asikhofu kuhusu hilo.

Hayo Ömer Çelik ameyasema akiwaambia waandishi wa habari jijini Istanbul.

Çelik alisema rais Recep Tayyip Erdoğan amedhamirşa kuitatua kesi hii kwa namna yeyote ile.

Ameongeza kuwa Uturuki haiwezi kumlaumu mtu yeyote kabla ya kumaliza uchunguzi, lakini baada ya uchunguzi kukamilika hakuna kitachofichwa.

Alisema pia ulimwengu mzima unafuatialia tukio hili hili kwa kuguswa mno na wanasifu mamlaka ya Uturuki kwa kazi nzuri inayoifanya katika uchunguzi  kufuatia tukio hilo.

 Habari Zinazohusiana