Hikaya za Anatolia

Hikaya za Anatolia,Kapadokya

Hikaya za Anatolia

Leo tutawaletea moja ya  hazina zilizopo ndani ya  Anatolia ambazo zimekua kivutio cha wengi duniani. Si kitu kingine bali ni miamba dohani iliyopo mjini Kapadokya, mji unaopatikana baina ya miji ya Kayseri, Nevşehir na Kirşehir karibu kabisa na mto mwekundu. Miamba  hii iligunduliwa  na watembezi wa awali na kuamua kuandika  urithi huu wa dunia katika vitabu na hivyo kujulikana. Miamba hii ya asili ilitokana na mmomonyoko ulosababishwa na maji na upepo ulovuma na kuacha miamba hii ikiwa imesimama mithili ya koni kwa maelfu ya miaka. Kwa mujibu wa wasafiri wa Ulaya miamba hiyo ilikua ni makazi ya dohani. Na ndio maana ikaitwa dohani. 

 

Neno Kapadokya liliwekwa na Wafarsi ambao walikiteka eneo hilo mnamo karne ya saba kabla ya kristu. Tangu siku hiyo mpaka sasa eneo hili linajulikana hivo na limevutia watalii wengi sana kulitembelea. Na sasa tuangalie kwa undani hazina hii iliyopo Kapadokya. 

 

Hapo zamani za kale, watu waliishi na watu wakubwa na waajabu. Ukubwa wa watu hawa uliwaletea woga wakazi na kukosa utulivu na amani. Lakini hawakuonesha hali hii kwasababu walihofia kuwakasirisha. Walikua wakikusanyika juu ya miamba ya dohani kuomba dua dhidi ya viumbe hawa. Wakati mwingine walipokasirika walikua wakirusha moto katika nyumba za watu waloishi eneo hili kutoka katika miamba hii ya dohani. Nyumba, mashamba na maeneo ya watu yalikua yakiungua na kuleta hasara kubwa. Naam ndipo viumbe wema walipokuja katika eneo hili. Walipoona yaliyokua yakifanywa na watu hawa wa ajabu dhidi ya wakazi wa kapadokya walichukia sana. Ndipo wakaamua kuwasaidia watu.

 

Cha kwanza walichofikiri ilikua ni kuuzima moto ambao ndio ilikua silaha kubwa ya majitu haya yaajabu. Kwa ruhusa ya mfalme, waliweka theluji juu ya miamba ya dohani katika matanuru ya moto yalokua yameandaliwa na watu hawa wa ajabu. Baada ya siku kadhaa malengo yao yakatimia. 

 

Majitu haya makubwa yalipoelewa kwamba hawawezi kupambana na viumbe wema walokuja kusaidia watu waliamua kuondoka na kuliacha eneo hilo. Wakazi hawa wakaanza kuishi kwa pamoja na kwa furaha. Watu waliwapenda sana viumbe hawa wema waliowaletea amani na utulivu. Wakawa wanaishi nao makazini kwao. Baadhi ya watu walianza kuoana na viumbe hawa. Baadhi ya watu walipinga jambo hili. Na ikafikia hatua ya vita baina yao. Viumbe hawa kwakua walimpenda sana mfalme, wakaona ni vema kuondoka eneo hilo ili kuepusha ugomvi baina yao na watu. 

 

Kisa kingine kizuri mnachoweza kukipata kuhusiana na miamba hii ya dohani mitatu inayofuatana. Inasemekana kwamba binti mfalme alimpenda mchunga mbuzi mmoja kijijini hapo. Mfalme alichukia Sana mapenzi haya kiasi akawatuma askari wake kwenda kumuua mchungaji huyu na baba yake. Binti mfalme alifahamu fika kuwa askari wale watawakamata mchungaji na baba yake pindi watakapojaribu kutoroka. Basi binti mfalme akaomba kwa mungu kwamba wabadilike na kuwa miamba ya dohani inayofuatana, endapo wote watauawa na askari hao. Na ndipo ilipotokea miamba hii. Na sehemu hii ya miamba huwa inatembelewa na watalii wengi sana. Na katika vivutio vizuri kabisa kwa wapanda parachuti ni miamba hiiHabari Zinazohusiana